Batshuayi aifungia Dortmund mabao mawili mechi yake ya kwanza

Michy Batshuayi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michy Batshuayi

Mshambuliaji wa Chelsea aliyeelekea katika klabu ya Borussia Dortmund kwa mkopo Michy Batshuayi alifunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza na klabu yake mpya dhidi ya Cologne.

Batshuayi, ambaye alielekea Dortmund hadi mwisho wa msimu huu alifunga bao lake la kwanza katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza bao la pili baada ya saa moja .

Mabao hayo mawili yalijiri baada ya bao la Simon Ziller kabla ya Jorge Mere kuwasawazishia wenyeji.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michy Batshuayi aifungia Dortmund mabao mawili katika mechi yake ya kwanza

Lakini baadaye Batshuayi alimpigia pasi nzuri Andre Schurrle aliyefunga bao la tatu na kuipatia ushindi Dortmund.

Ushindi huo unaipeleka Dortmund hadi nafasi ya pili katika ligi ya Bundesliga.

Mada zinazohusiana