Maradona anyimwa visa ya kuingia Marekani kwa kumtusi Trump

Maradona anyimwa visa ya kuingia Marekani kwa kumtusi Trump
Maelezo ya picha,

Maradona anyimwa visa ya kuingia Marekani kwa kumtusi Trump

Nyota wa zamani wa soka nchini Argentina Digo Maradona amenyimwa kibali cha kuingia nchini Marekani baada ya kudaiwa 'kumtusi' rais Donald Trump katika runinga.

Maradona alitarajiwa kusafiri kuelekea Miami kushiriki katika kusikilizwa kwa kesi ya mkewe wa zamani .

Lakini Maradona ambaye anasimamia klabu ya UAE ya Al Fujairah amekatazwa visa kwa mara nyengine kuingia Marekani.

Katika mahojiano Maradona anadaiwa kumuita Trump 'Chirolita'.

Neno hilo ni tusi linalojulikana sana nchini Argentina likimaanisha watu ambao ni vikaragosi.

Wakili wa Mardona Matias Morla sasa atamwakilisha mtaja wake katika kesi hiyo mjini Miami.