Alexis Sanchez aisaidia Man United kushinda huku ManCity ikizuiwa

Kiungo wa kati wa Man United Alexi Sanchez akifunga mkwaju wa penalti Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiungo wa kati wa Man United Alexi Sanchez akifunga mkwaju wa penalti

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amekataa kumlaumu Raheem Sterling kwa mkosi wa kikosi chake kushindwa kuilaza Burnley baada ya mshambuliaji huyo wa Uingereza kukosa nafasi ya pekee.

Huku ikiwa 1-0 na dakika 20 chini ya ushindi wao wa 23 msimu huu, Sterling alishindwa kucheka na wavu akiwa maguu sita baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Kyle Walker.

Kisa hicho kilimfanya kuzomwa huku mchezaji huyo akitolewa mara moja kabla ya Johann Berg Gudmundsson kuisawazishia Burnley ikiwa zimesalia dakika nane.

Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche alihisi kushindwa huko kwa Sterling kulibadilisha hali ya mechi hiyo.

Uwanja mzima ulianza kutushangilia.

Lakini Guradiola amesisitiza kuwa hakumtoa nje Sterling kwa sababu ya kukosa nafasi hiyo ya wazi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amekataa kumlaumu Raheem Sterling kwa mkosi wa kikosi chake kushindwa kuilaza Burnley

Wakati huohuo Alexis Sanchez alifunga bao lake la kwanza akiichezea Manchester United baada ya timu hiyo kuishinda Huddersfield na hivyobasi kuisukuma katika eneo la kushushwa daraja.

Baada ya kipindi cha kwanza Romelu Lukaku aliipatia United uongozi kunako dakika 55 baada ya kupokea krosi nzuri.

Sanchez baadaye alichezewa rafu na beki wa Huddersfield Michael Hefele na hivyobasi kutunukiwa mkwaju wa penalti aliopiga ukapunguliwa na kipa kabla ya kuupata na kufunga.

Matokeo mengine:

  • Bournemouth 2-1 Stoke City
  • Leicester 1-1 Swansea
  • Brighton 3-1 West Ham
  • Leicester 1-1 Swansea
  • West Brom 2-3 Southampton

Mada zinazohusiana