CHAN 2018: Sudan yaibuka ya tatu baada ya kuishinda Libya kwa penalti

Chan logo Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Libya na Sudan ziliishindania nafasi ya tatu katika CHAN huko Marrakech Jumamosi

Kipa wa Sudan Akram El Hadi aliokowa mikwaju miwili ya penalti wakati timu yake ilipoishinida Libya na kuibuka nafasi yatatu katika mashindano ya ubingwa wa mataifa ya Afrika (CHAN).

Mechi ilimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 huko Marrakech.

Awali Akram alishindwa kuihimili krosi kutokakwa Salem Ablo iliochangia sare hiyo kwa Libya zikiwa zimesalia dakika sita tu kwa mechi kuisha.

Sudan iliongozwa kunako dakika nane wakati Walaa Eldin Musa alipotikiza wavu kutokana na hedi aliyoipiga.

Katika awamuya mikwaju ya penalti , Sudan ilifanikiwa kusukuma mikwaju yote minne ndani huku mikwaju ya Elmehdi Elhouni na Ablo ikizuiwa na Akram.

Ni shaba ya pili kwa Sudan katika fainali za mshindani hayo ya CHAN baada ya kuibuka tena nafasi ya tatu walipokuwa waandalizi wa mashndano hayo mnamo 2011, huku Libya wakiibuka mabingwa miaka mitatu baada ya hapo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii