Tetesi za soka Jumatatu 5.02.18

EPL Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere

Klabu ya Liverpool itaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, kama mchezaji huyo atagoma kusaini mkataba mpya na klabu yake.

Manchester United wanamfutilia kwa karibu kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic ili kuweza kumsajili kiungo huyo katika dirisha kubwa la usajili.

Mshambuliji wa Man United Marcus Rashford anaweza kuondoka klabuni hapo ikiwa United wa tamsajili Justin Kluiverts kutoka Ajax.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Winga wa Bordeaux Malcom Oliveira

Mshambuliaji wa Kibrazil Malcom Oliveira, anataka kuondoka katika klabu yake ya Bordeaux, na Mchezaji huyo anawinda na Tottenham na Arsenal

Mshambuliji wa West Ham Javier Hernandez, 29, amesema atajitoa kwa asilimia mia moja katika klabu yake licha ya kutaka kuondoka klabuni hapo katika dirisha la mwezi januari

Mfaransa Olivier Giroud mwenye miaka 31 ambae anaweza anza katika mchezo wa timu yake mpya ya Chelsea itapocheza na Watford amesema alipewa motisha ya kuhama na kocha wa timu ya taifa ya ufaransa Didier Deschamps.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji mpya wa Chelsea Olivier Giroud

Winga wa Leicester Marc Albrighton amekanusha taarifa zinazozagaa mitandaoni kuwa wachezaji wa Foxes wanahasira na mchezaji mwenzao Riyad Mahrez aliyetaka kuhama na kujiunga na Man City.

Meneja wa Manchester United hana mpango wa kumsajili mchezaji wa idara ya ushambuliaji katika dirisha lijalo la usajili kwa kuwa ana furaha na ukubwa kikosi alichonacho.

Kiungo wa Chelsea Danny Danny Drinkwater amesema mchezaji mwenzake Eden Hazard na Paul Scholes ndio wachezaji bora aliwahi kucheza nao.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Drinkwater

Mada zinazohusiana