Chelsea iko ugenini leo kuwakabili Watford

EPL Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kikosi cha Chelsea

Ligi kuu ya England itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa bingwa mtetezi wa ligi Chelsea atakuwa ugenini katika dimba la Vicarage Road kucheza na wenyeji wao Watford.

Mchezo huu ni wa raundi ya ishirini na sita, Watford, chini ya kocha wake Javier Gracia, huenda wakamkosa kiungo wake Tom Cleverley ambae ni majeruhi na pia watamkosa mchezaji wao mpya Didie Ndong.

Chelsea wanatarajia kuwatumia wachezaji wake wapya mshambuliaji Olivier Giroud na Emerson Palmieri, huku kiungo Willian na David Luiz wakijumuishwa kuwa sehemu ya timu baada ya kutoka kwenye majeraha.

Beki Andreas Christensen hatima yake bado inamashaka kucheza mchezo huo kutoka na kuumia katika mchezo dhidi ya Bournemouth, nae Alvaro Morata anaendelea na matibabu ya maumivu ya mgongo.

Mada zinazohusiana