Man City kucheza na Birmingham raundi ya tano FA ya wanawake

Fa Cup
Image caption Bingwa mtetezi wa kombe la FA Manchester City

Ratiba ya raundi ya tano ya kombe la Fa Kwa wanawake nchini England imetoka bingwa mtetezi Manchester City waanza kwa kusafiri kwenda kucheza na Birminghama City.

Mabingwa mara 14, wa michuano hiyo klabu ya Arsenal wao watakuwa wenyeji wa klabu ya Millwall, Chelsea watacheza na timu ya Doncaster Rovers Belles.

Michezo ya raundi ya tano ya kombe la FA, ambayo imebakiza jumla ya vilabu 16 itachezwa jumapili ya Februari 18.

Ratiba kamili ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo

Arsenal v Millwall Lionesses

Cardiff City v Charlton

Lewes v Everton

Sunderland v Aston Villa

Chichester City v Liverpool

Birmingham City v Manchester City

Chelsea v Doncaster Rovers Belles

Durham v Plymouth Argyle or Leicester City

Mada zinazohusiana