Cameroon Mwenyeji wa Afcon 2019

CAF yapitisha Cameroon mwenyeji mashindano ya Afcon 2019
Image caption CAF yapitisha Cameroon mwenyeji mashindano ya Afcon 2019

Baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya Cameroon kuwa wenyeji wa fainali za AFCON mwaka 2019 michuano ambayo inayotarajiwa kuanza June saba hadi Julai saba, kutokana na kutokuwepo kwa kimiundombinu mizuri na maswala ya uchumi kuweza kuandaa michuano hiyo , CAF ililazimika kufanya uchunguzi wa maandali zi hayo.

Baada ya CAF kumaliza kufanya uchunguzi hatimaye wametoa ruhusu kwa Cameroon kuendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo baada ya timu ya maafisa wa CAF kuridhishwa na maandalizi yanayoendelea nchini humo.

Juniour Binyam ni mwenyekiti wa kamati ya masuala ya habari wa CAF amethibitisha hilo na kusema kwamba CAF kwa sasa hawana mashaka juu ya maandalizi ya michuano hiyo na wanaona hadi kufika wakati huo Cameroon watakuwa tayari.

Inatajwa moja ya sababu kubwa iliyokuwa inatoa mashaka kwa CAF kuto waamini sana Cameroon ni kutokana na ongezeko la timu kutoka 16 kwenda hadi 24 jambo ambalo ilidhaniwa inaweza kuwa sumbua Cameroon lakini wanaonekana wanaweza kukabiliana nalo.

Mada zinazohusiana