Tetesi za soka Ulaya Jumanne 06.02.2018

Pierre Emerick Aubameyang
Image caption Pierre Emerick Aubameyang

Afsa mkuu mtendaji wa klabu ya Dortmund Hans-Joachim Watzke amemshutumu mshambuliaji mpya wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang kwa kudai kwamba hakucheza kwa kiwango chake cha juu alipokuwa akijaribu kulazimisha uhamisho wake kuelekea Arsenal .(Mirror)

Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, anasema kuwa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 29, ndiye mchezaji aliyefaa kusajiliwa na Manchester United kutokana na ukakamavu wake, upendo na tamaa alionayo.(Express)

Image caption Hary Kane akiwa kijana mdogo aliichezea Arsenal

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane anasema kuachiliwa na Arsenal akiwa na umri wa miaka 9 ndio kitu bora kilichofanyika kwake. (London Evening Standard)

Kipa wa Uingereza Joe Hart ananyatiwa na Chelsea iwapo kipa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 25 Thibaut Courtois ataelekea Real Madrid. Hart, 30,kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya West Ham kutoka Manchester City. (Sun)

Image caption David Moyes

Mkufunzi wa West Ham David Moyes huenda asiendeleze mkataba wake katika klabu ya West Ham baada ya msimu huu iwapo klabu hiyo itasalia katika ligi ya Uingereza au la. (Telegraph)

Arsenal inataka kumzuia Aaron Ramsey kwa mktaba mpya wa kudumu. Kandarasi ya raia huyo wa Wales inakamilika katika kipindi cha miezi 18 ijayo. (Mirror)

Image caption Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha atahitaji mtaalam wa upasuaji wa goti lake baada ya kupata jeraha kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle siku ya Jumapili.

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha atahitaji mtaalam wa upasuaji wa goti lake baada ya kupata jeraha kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle siku ya Jumapili.

Mchezaji huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kutocheza kwa hadi kipindi cha wiki nne. (Guardian)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United inatarajiwa kushindana na Liverpool na Bayern Munich katika kumwania winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 9 raia wa Marekani Christian Pulisic. (Bild - in German)

Mshambuliaji wa Crystal Palace Winfried Zaha na mkufunzi Roy Hodgson wameorodheshwa miongoni mwa watu ambao watazawadiwa tuzo katika tamasha la tuzo za kandanda mwaka huu mjini London (Croydon Advertiser)

Manchester United inatarajiwa kushindana na Liverpool na Bayern Munich katika kumwania winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 9 raia wa Marekani Christian Pulisic. (Bild - in German)

Image caption Manchester United itafanya mkutano na mashabiki wake baada ya mkufunzi Jose Mourinho kulalamika kuhusu kimya kilichofuatia baada ya ushindi dhidi ya Huddersfield siku Saturday. (Star)

Manchester United itafanya mkutano na mashabiki wake baada ya mkufunzi Jose Mourinho kulalamika kuhusu kimya kilichofuatia baada ya ushindi dhidi ya Huddersfield siku Saturday. (Star)

The Red Devils pia wamemfanyia majaribio kijana wa Colombia Wilson Tilve, 16, ambaye amefananishwa na kiungo wa kati wa Bayern James Rodriguez. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, anasema kuwa atakuwa mkufunzi baada ya kustaafu kucheza kandanda. (Sky Sports)

Image caption Vincent Kompany

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amemuhakikishia nahodha wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 31 Vincent Kompany kwamba bado ana fursa ya kucheza katika mpango wa kuwania mataji manne.(Manchester Evening News)

Itali imekubali kushindwa katika jaribio lao la kutaka kumshawishi mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte kuwa meneja wa timu ya taifa kwa mara ya pili. (London Evening Standard)

Image caption Mkufunzi wa zamani wa Everton Ronald Koeman

Mkufunzi wa zamani wa Everton Ronald Koeman atazinduliwa kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Uholanzi siku ya Jumanne(De Telegraaf - in Dutch)

Kiungo wa kati wa zamani wa Real Madrid na AC Milan Clarence Seedorf ametajwa kuwa mkufunzi wa klabu ya Deportivo La Coruna.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 na raia wa Uholanzi atasimamia timu hiyo kwa kipindi cha msimu uliosalia baada ya kufutwa kwa mkufunzi Cristobal Parralo(Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Feyenoord raia wa Denmark Nicolai Jorgensen

Mshambuliaji wa Feyenoord raia wa Denmark Nicolai Jorgensen, 27, ambaye amekuwa akisakwa na Newcastle katika dirisha la uhamisho la mwezi uliopita amesema kuwa yuko tayari kuelekea katika klabu hiyo ya Uingereza mwishoni mwa msimu huu(Newcastle Chronicle)

Kiungo wa kati wa Newcastle Jack Colback, 28, ambaye anahudumu kipindi kilichosalia cha msimu kwa mkopo katika klabu ya Nottingham Forest, amemshutumu mkufunzi wa klabu hiyo Rafael Benitez kwa 'kutomuheshima' kwa kumfanya afanye mazoezi na timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 baada ya kuamua kwamba hayuko katika mipango yake ya muda mrefu.. (Express)

Nahodha wa Stoke Ryan Shawcross, 30, ametaja mechi dhidi ya Brighton siku ya Jumamosi kuwa mechi kubwa ya msimu (Argus)

Mada zinazohusiana