Bondia Muhammad Ali afungiwa miaka miwili

Boxing Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bondia Muhammad Ali amefungiwa kwa miaka miwili

Bondia Muhammad Ali, raia wa uingereza amefungiwa kwa miaka miwili kujihusisha na mchezo wa masubwi baada ya kushindwa vipimo vya dawa zilizokatazwa michezoni.

Ali mwenye miaka 21, alishindwa kufaulu vipimo alipokua nashikiriki michezo ya dunia ya masubwi iliyofanyika nchini Morocco mwaka jana.

Bondia huyo alisimamishwa toka mwezi octoba mwaka jana na amefikia makubaliano ya kukubali adhabu hiyo na chama cha kimataifa cha mchezo wa ndondi. (AIBA).

Vipimo vinaonyesha bondia huyu amekuwa akitumia dawa aina ya Trenbolone, ambazo hutumika kukuza na kusisimua misuli na dawa hizo zimekatazwa michezoni na Wada.

Mada zinazohusiana