Tetetsi za soka Ulaya na Afrika mashariki Jumatano 07.02.2018

Mkufunzi wa Cheslea Antonio Conte
Image caption Mkufunzi wa Cheslea Antonio Conte

Aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Luis Enrique ni miongoni mwa makocha walioorodheshwa na mmiliki wa timu hiyo Roman Abrahamovic kuchukua mahala pake mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte iwapo atafutwa kazi. (Sport - in Spanish)

Enrique ambaye ni raia wa Uhispania inadaiwa atamsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez iwapo atasajiliwa kuifunza The Blues. (Le10Sport - in French)

Mechi kali inatarajiwa kati ya Njombe Mji na Young Africans katika uwanja wa Uhuru . Mchezo wa Yanga umeimarika pakubwa katika siku za hivi karibuni. Walisitisha matumaini ya klabu ya Azam ya kukamilisha msimu mzima bila kupoteza mechi wakiwashinda 2-1 katika uwanja wa Azam katika mechi mbili za mwisho ilizocheza.{The Citizen Tanzania}.

Hatahivyo, Enrique hayuko tayari kukatiza likizo yake kutoka katika soka na kwamba yuko tayari kuchukua kazi hiyo mwisho wa msimu huu.(Goal)

Image caption Aliyekuwa kocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte analipia makosa yaliofanywa na mkurugenzi wa zamani wa kiufundi katika klabu hiyo Michael Emenalo katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu uliopita kulingana na mchezaji wa zamani na naibu mkufunzi Ray Wilkins. (talksport)

Conte amesalia na miezi 18 katika kandarasi yake na kwamba hatowacha kazi (Mirror)

Image caption Mmiliki wa klabu ya Chelsea Abramovich

Abramovich hatoruhusu wachezaji kuamua iwapo Conte anfaa kusalia katika uwanja wa Stamford Bridge. (Telegraph)

Mabingwa wa zamani wa ligi nchini Kenya AFC Leopards wanaelekea mjini Kakamega siku ya Jumatano ili kujiandaa tayari kwa mechi yake ya kombe la Caf .

Mabingwa hao wa kombe la Gotv wataikaribisha nyumbani klabu ya Madagascar Fosa juniors katika awamu ya kwanza katika uwanj wa Bukhungu siku ya Jumapili.Awamu ya pili ya mechi ya marudiano inatarajiwa kufanyika wiki moja baadaye nchini Madagascar.{Nation Daily Newspaper}

Image caption Kipa wa Chelsea na Ubelgiji Thibaut Courtois

Kipa wa Chelsea na Ubelgiji Thibaut Courtois, 25, anasema hali yake huenda ikamruhusu kuelekea klabu ya Real Madrid iwapo mabingwa hao wa Ulaya wataonyessha hamu ya kutaka kumsajili. (Sport Foot Magazine, via Daily Mail)

Kipa wa Manchester United David de Gea atasalia kuwa kivutio kwa Real Madrid' katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu, lakini United inatarajiwa kumpatia raia huyo wa Uhispania mkataba mpya. (Sport - in Spanish)

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda Cranes, Isaac Isinde na Boban Zirintusa wameachiliwa na klabu ya Zambia Buildcon FC. Isinde na Zirintusa ni miongoni mwa wachezaji 16 ambao klabu hiyo imewatoa.{New Vision Uganda}

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal wana hamu ya kumsajili beki wa Juventus Daniele Rugani

Arsenal wana hamu ya kumsajili beki wa Juventus Daniele Rugani, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo wa miaka 23 kutoka Itali. (Star)

Liverpool Itamtoa kwa mkopo beki wa Colombia mwenye umri wa miaka 18 Anderson Arroyo kwenda Real Mallorca baada ya kupokea nakala za kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Fortaleza CEIF. (Liverpool Echo)

Kipa wa Roma Alisson, anayelengwa na Liverpool, ni kipa bora zaidi duniani na raia huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 ana thamani ya Yuro 50m kulingana na kocha Roberto Negrsolo. (Il Romanista, via Goal)

Image caption El Hadji Diouf

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Bolton, Sunderland, Blackburn na Leeds El Hadji Diouf, 37, anataka kuwa mwanasiasa nchini Senegel.(FourFourTwo)

Klabu ya Benevento, ambayo iko pointi tisa chini ya ligi ya Serie A , imefanya majaribio ya kuwasajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Samir Nasri na Alex Song, wote wakiwa na umri wa 30, na wako huru. (Sky Italia - in Italian)