Tetesi za soka Ulaya na Afrika mashariki Alhamisi 08.02.2018

Ni kiungo wa kati wa Monaco anayenyatiwa na Liverpool
Image caption Thomas Lemar

Liverpool inajiandaa kwa jaribio la pili kumsajili kiungo wa wakti wa Monaco mwenye umri wa miaka 22 Thomas Lemar wa Ufaransa baada ya kukataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza.

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola hatoanzisha tena harakati za kutaka kumsajili winga wa Leicester raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 26 Riyad Mahrez mwishoni mwa msimu huu. (mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ambaye anahusishwa na kuchukua mahala pake Antonio Conte wa Chelsea anajiandaa kuelekea nchini Uingereza.

Image caption Aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Louis Enrique

Hatahivyo mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 47 hataki kumrithi Conte hadi mwisho wa msimu huu.

Obrey Chirwa amempiku John Bocco katika harakati za kushinda taji la mfungaji bora katika Ligi Kuu Bara, Lakini Okwi bado ndiye aliye juu kwa mabao.

Chirwa aliyeanza wiki akiwa na mabao sawa na mshambuliaji wa Simba alifunga hat-trick kaytika mchuano kati ya yanga na Njombe mji katika uanwja wa kitaifa.

Image caption Abdoulaye Doucoure kulia

Tottenham inataka kumsaini kiungo wa kati wa Watford na Ufaransa Abdoulaye Doucoure mwishoni mwa msimu huu.

Beki wa Brazil Fabinho mwenye umri wa miaka 24 ambaye klabu ya Manchester United ilikuwa inamnyatia msimu uliopita anasema kuwa muda wake katika klabu ya Monaco unakamilika(Metro)

Image caption Lionel Messi

Klabu ya ligu kuu nchini China Hebei China Fortune inajiandaa kuwasilisha ombi jingine kwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 30, baada ya ombi lao la kwanza kukataliwa. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred amechagua klabu ya Manchester City kama klabu anayopanga kuhamia , kulingana na mkufunzi wa zamani Mircea Lucescu.

Raia huyo wa Brazil mwenye umri wa 24 pia amehusishwa na majirani wa City Manchester United. (Mirror)

Mkufunzi wa timu ya taifa ya Uganda Cranes Moses Basena na Fred Kajoba wanatarajiwa kuelekea nchini Marekani kwa mafunzo ya soka kaytika klabu ya York Red Bulls.

Wawili hao walitarajiwa kuelekea mjini New York tarahe 6 Februari kwa mafunzo ya mwezi mmoja , lakini safari yao imepelekwa mbele na sasa watakwenda tarehe 10 mwezi Machi huku wawili hao wakipewa fursa ya kujifunza zaidi kuhusu mnbinu za ukufunzi.

Image caption Mshambuliaji wa Itali Fabio Borini

Mshambuliaji wa Itali Fabio Borini na winga wa Uholanzi Jeremain Lens wataondoka Sunderland mwisho wa msimu huu baada ya kubadilisha vifungu vya sheria katika mkataba wao ambapo vinalazimu klabu zilizowasajili kwa mkataba wa muda kuwanunua.

Wako katika mkopo katika klabu za AC Milan na Besikitas mtawalia. (Northern Echo)

Nottingham Forest inajiandaa kumsajili kipa wa Ugiriki Stefanos Kapino. Mchezaji huyo mwnye umri wa miaka 23 aliondoka katika klabu ya Olympiakos iliokuwa ikimilikiwa na mmiliki wa sasa wa klabu ya Forest Angelos Marinakis baada ya migogoro kadhaa (Sun)

Image caption Mshambuliaji Benik Afobe

Mshambuliaji Benik Afobe, 24, atarudi katika klabu ya Wolvehampton kwa kandarasi ya kudumu iwapo viongozi hao wa ligi ya daraja la kwanza Uingereza watapandishwa katika ligi ya Premia.

Aliondoka katika klabu ya Molineux ili kujiunga na Bournemouth mwezi Januari 2016 lakini akarudi kwa mkopo mwezi Januari. (mirror)

Mshambuliaji wa Arsenal Striker Pierre-Emerick Aubameyang, 28, anasema kuwa alijiunga na Arsenal mwezi Januari baada ya kupigiwa simu na mchezaji wa zamani wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan. (Sky Sports)

Klabu za K'Ogalo {Gor Mahia} na Ingwe{Leopard} nchini Kenya zina fursa nyengine kuthibitisha thamani yao katika soka ya kimataifa barani Afrika wakati watakapocheza nyumbani.

Image caption Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo, 33, anasema kuwa anaweza kuendelea kucheza kwa kipindi cha muda mrefu ujao.. (GQ - in Italian)

Beki wa Manchester United Luke Shaw anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya mwishoni mwa msimu huu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles

Arsenal imeanza mazungumzo na kiungo wa kati Ainsley Maitland-Niles kuhusu mkataba mpya. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kutolka uingereza amesalia na miezi 18 mkataba wake kukamilika. (ESPN)