Wenger: Wachezaji wa Uingereza ni 'mabingwa' wa kujiangusha uwanjani

Arsene Wenger alalama huu ni mchezo mchafu
Maelezo ya picha,

Arsene Wenger alalama huu ni mchezo mchafu

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amelalamika kwamba wachezaji wa Uingereza wamekuwa na tabia ya kujirusha na kutengeneza adhabu. Amesema mchezaji wa Tottenham Dele Alli alifanya kitendo hicho kwenye mchezo wa jumapili huko Liverpool na kusababisha mwamuzi kutoa adhabu ya penalti.

Mchezaji mwingine ambaye anatuhumiwa kufanya kitendo hicho ni Harry Kane, alifanya hivyo kwa mchezaji Virgil van Dijk wa Liverpool na kusababisha mpira wa adhabu

Wenger amesisitiza kwamba anakumbuka kumekuwa na kesi za wachezaji kutoka nje ya Uingereza, lakini wachezaji wa Uingereza sasa wameiga tabia hiyo na wamekuwa vinara wa matukio hayo kuliko wachezaji wengine.