Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 09.02.2018

Bundesliga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliji wa Borusia Dortmund Christian Pulisic,

Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Christian Pulisic, 19, amekataa kupinga uhamisho wa kuelekea katika klabu ya Manchester United, Klabu aliyokuwa akiishabikia akiwa mtoto. (Mail)

Winga wa Leicester na Algeria mwenye umri wa miaka 26 Riyad Mahrez anataka klabu yake kumuhakikishia kuwa ataruhusiwa kuondoka mwisho wa msimu huu kabla ya kurui katika mamzoezi.. (Times - subscription required)

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere atalazimika kupunguza mshahara wake ili kutia saini mkataba mpya (Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette yuko chini ya presha katika uwanja wa emirates na huenda akaondoka mwisho wa msimu huu kulingana na mchezaji wa zamani wa Arsenal Emmanuel Petit.(Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette

Washauri wa Mahrez wanadai Leicester walikuwa tayari wamekubali kumruhusu kuondoka iwapo klabu kubwa ingetoa dau la £50m lakini bado ikakataa ombi la klabu ya Manchester City mwezi Januari. (Mirror)

Mkufunzi wa Ujerumani Joachim Low ndio anayelengwa na Real Madrid kuchukua mahala pake Zinedine Zidane kama mkufunzi mwishoni mwa msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mkufunzi wa zamani wa Watford Marco Silva ameitishia klabu hiyo na hatuakali za kisheria kwa kuwa bado anasubiri kulipwa fidia baada ya kufutwa kazi mnamo mwezi Januari.(Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Ufaransa na Monaco Thomas lemar 22 hayuko katika orodha ya Liverpool ya uhamisho katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu(Liverpool Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Thomas Lemar

Juventus wanauhakika wa kumsajili kiungo wa Liverpool Emre Can,wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu(Mirror)

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski amesema tetesi za kuwa atajiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu tetesi hizo hazimvutii (Bild - in German)

Leicester na West Ham wako katika mvutano wa kumuwania kinda Patrick Roberts ambae anakipiga kwa mkopo katika klabu ya Celtic akitokea Manchester City. (Sun)

Winga wa zamani wa Manchester United Angel Di Maria, 29, amekiri ilibaki kidogo aondoke Paris St. Germain na kujunga na Barcelona katika dirisha kubwa la usajili lilipita(Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Angel De Maria amesema alikaribia kujiunga na Barcelona

Klabu ya Barnsley inamtaka meneja wa Peterborough United kwenda kuziba pengo la Paul Heckingbottom,ambae ameikacha klabu hiyo na kujunga na Leeds. (Telegraph)

Mchezaji wa zamani wa Arsenal and Tottenham mlinzi Sol Campbell amefanya mazungumzo na Oxford ninayoshiriki ligi one inayotaka kumchukua kama kocha wa kikosi hicho. (Mail)