Tottenham yailaza Arsenal 1-0

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs akifunga bao lililoipatia ushindi timu yake dhidi ya Arsenal

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs akifunga bao lililoipatia ushindi timu yake dhidi ya Arsenal

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ndiye anayeshikilia hatma ya klabu hiyo kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Mauricio Pochettino, kufuatia mchezo wake uliosaidia timu hiyo kuwalaza maadui zao wa mjini London.

Kichwa kikali kilichopigwa na Kane kilimwacha kipa Petr Cech bila jibu na kutingisa wavu katika mechi hiyo ya debi ya London inayoiweka Hotspurs katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi.

Kane Aliruka juu ya beki wa Arsenal Laurent Kolscieny katika dakika ya 49 na kufunga krosi iliopigwa na Ben Davie .

Na ulindaji lango mzuri wa Cech ulioweza kuizuia Spurs katika kipindi cha pili, akipangua mashambulio kadhaa na hivyobasi kuiweka Arsenal katika mchuano huo.

Mchezo wa Tottenham iliotawala kila safu uliwawacha wachezaji wa Arsenal mdomo wazi huku mchezaji wa ziada Alexandre Lacazette akikosa nafasi mbili za wazi, mojawapo akiwa amesalia na kipa Hugo Lloris na kupiga nje.