Mourinho: Hatungefunga bao hata kama tungecheza kwa saa kumi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mourinho: Hatungefunga bao hata kama tungecheza kwa saa kumi
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa klabu yake haingefunga bao hata kama ingecheza kwa saa kumi baada ya upande wake kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Newcastle.
Bao la dakika ya 65 la Matt Ritchie lilisababisha The Red Devils kushindwa kwa mara ya tano msimu huu.
Sasa Manchestrer United wako nyuma ya viongozi Manchester City kwa pointi 16.
"Miungu yao ya kanndanda ilikuwa wazi nao," aliseam Mourinho. "Haingewezekana leo."
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea alisema kuwa Newcastle walicheza kama wanyama kushinda nyumbani kwa mara ya kwanza tangu Oktoba.
Chanzo cha picha, Getty Images
Alexis Sanchez alikosa nafasi nzuri
"Hisia zangu ni kuwa tungecheza kwa saa 10 na hatungefuga bao," alisema.
"Tulikuwa na fursa wakati tulikuwa 0-0, alisema Mourinho, Alexis Sanchez alikuwa na fursa ya kufunga na kisha fursa zingine dakika za 20 na 25 za mwisho
Free-kick ambayo ilichangia bao lake Ritchie, iliptikana wakati beki wa Manchester United Chris Smalling alilaumiwa kwa kuruka.