Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 12.02.2018

Haki miliki ya picha Huw Evans picture agency
Image caption Fernando Llorente

Mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld hawezi kusafiri kwenda Turin kwa mechi ya ligi ya mabingwa na Juventus halia ambayo inaweka hamtma yake katika klabu hiyo kuwa yenye utata.

Mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente, 32, ametilia shaka hatma yake huko Tottenham akikiri kuwa ameokosa Juventus. (Mirror)

Kocha wa Chelsea Antonio Conte anasema wachezaji wake hawaathiriki kwa vyoyote na uvumi unazunguka hatma yake klabuni. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Antonio Conte

Chelsea wanaangalia uwezekano wa kumfuta Conte na mahala pake kumleta aliyekuwa meneja wa Watford Marco Silva katika mkataba wa muda. (Times)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kuwashinda Manchester City katika kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco. (Star)

Real Madird watamwendea kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, 25, baada ya kuamua kuwa itakuwa rahisi kumsaini kuliko Mhispania mweye umri wa miaka 27 David de Gea kutoka Manchester United. (Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marcelo-kulia

Beki wa Real Madrid Marcelo anaamini kuwa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, atajiunga na klabu hiyo siku za usoni na anaamini kuwa ikiwa mbrazil huyo mwenzake atakuwa bora kwa klabu hiyo ya La Liga. (Marca)

Lakini beki wa PSG Thiago Silva anaamini kuwa Neymar atasalia katika klabu hiyo. (Canal+ via Goal)

Meneja wa West Brom Alan Pardew anatepeleka kikosi chake nchini Uhispani kwenye joyo kwa mazoezi wakati wanajaribu kuzuiz kuondolewa kutoka kwa Ligi. (Telegraph)

Mada zinazohusiana