Newcastle 1-0 Man Utd: Kwa nini Jose Mourinho alikosea, Newcastle haikua na bahati - Shearer

Mchezaji wa zamani wa Newcastle Allan Shearer
Image caption Mchezaji wa zamani wa Newcastle Allan Shearer

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho alikosea sana wakati aliposema kuwa Newcastle ilicheza ikipigania kupata sare na kwamba walitegemea bahati kuilaza Manchester United.

Kitu cha pekee ambacho Mourinho hakukosea wakati wa mahojiano baada ya mechi hiyo ni kwamba wachezaji wa Newcastle walifanya bidii kupata ushindi huo.

Kikosi hicho cha Rafa Benitez kilistahili ushindi kwa sababu kililinda lango lake vizuri ikilinganishwa na Manchester United , walitawala safu ya kati na walifanya kile ambacho United hawakuweza kufanya ambacho ilikuwa kufunga goli.

Ni kweli kwamba United ilitengeza nafasi chungu nzima na kwamba kipa wa Newcastle alikuwa na mchezo mzuri sana.

Lakini Mourinho anategemea kipa wake David de Gea kuwapatia pointi moja mara nyengine kama walivyocheza katika uwanja wa Anfield msimu huu ulipoanza kwa mfano.

Mourinho hawezikusema kwamba kulikuwa na utata katika matokeo hayo na ni hivyohivyo ambavyo Newcastle ilijipatia ushindi wake, walikuwa na bahati ni kweli.

Kuanzia mwanzo hadi mwisho, ilikuwa timu iliocheza katika kila safu, na ni makosa kulaumu upande mmoja kwa sababu klabu hiyo ilicheza vyema.

Kwa upande mwengine mechi hiyo ilionyesha ni kwa nini Manchester United wako nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City katika jedwali la ligi, kwa kuwa walishindwa kuonyesha mchezo mzuri katika safu zote.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption jedwali la ligi ya uingereza

Mashabiki wa Newcastle waliwashangilia wachezaji wao kutoka mwanzo

Newcastle ilikuwa chini ya jedwali la ligi kabla ya kuanza kwa mechi hiyo kutokana na ushindi wa Bournemouth dhidi ya Huddersfield mapema siku hiyo.

Swansea pia ilipanda juu ya Newcastle katika jedwali baada ya ushindi wao dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi, kwa hivyo ikawa muhimu kwamba walifaa kupata kitu katika mechi hiyo na walivyocheza walionyesha kwamba walitaka kupata kitu.

Mbali na kupata pointi tatu za kupanda katika jedwali, mchezo wao pia utawapatia motisha kitu ambacho wamekuwa wakikosa nyumbani na ndio sababu wamekuwa wakicheza vibaya.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Newcastle iko katika nafasi ya 13 katika jedwali lakini pia wako pointi mbili juu ya eneo la kushushwa daraja.

Mashabiki wa Newcastle waliisaidia timu yao lakini mchezo wa Newcastle dhidi ya Man united katika dakika 10 za kwanza ndio uliowafurusha walioingia katika uwnaja huo kuanzia mwanzo.

Benitez alicheza na wachezaji wawili mbele , Dwight Gayle na Ayoze Perez, ambao walitekeleza mashambulio kadhaa huku kasi ya kikosi chote cha Newcastle ikitawala kipindi chote cha mechi hiyo.

Tulikuwa tukijaribu kucheza kama hivyo nilipokuwa nikiichezea Newcastle kwa sababu tulijua iwapo tutashambulia itajenga hali nzuri ya mchezo na kupata motisha kutoka kwa mashabiki.

Naelewa ni kwa nini kikosi hiki cha Newcastle kimeshindwa kucheza hivyo mara kwa mara kwa sababu Benitez anajua uwezo wa kikosi alichonacho.

St James Park pia ni mazingira magumu kuchezea wakati huu kwa sababu ya kile kinachoendelea nyuma, huku mashabiki wengi wakitaka mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kuondoka.

Lakini sasa wachezaji wameonyesha ni nini wanaweza fanya na ni nini watakachopata watakapoonyesha mchezo mzuri.

Newcastle itahitaji kuonyesha mchezo mzuri nyumbani kama huu katika miezi kadhaa ijayo iwapo watasalia juu , na huku wakiungwa mkono na mashabiki wana fursa nzuri sana,

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Newcastle XI v Man Utd

Huku Dubravaska akiwa langoni, Jamaal Laschelles alionyesha mchezo mzuri naye Jonjo Shelvey na Mohamed Diame walitawala safu ya kati hadi pale Paul Pogba na Nemajna Matic wakalazimika kutolewa.

Newcastle ilikuwa na fursa nyingi za magoli-De Gea aliokoa shambulio la Shelvey na nusra wapate penalti wakati Chris Smalling alipomchezea visivyo Gayle.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Man Utd XI v Newcastle

Na wakati Manchester United walipoanza kuwashambulia Newcatsle waliweka ulinzi wa hali ya juu .

Kitu kimoja ambcho Benitez amekizungumzia sana katika safu ya nyuma ni ukosefu wa uzoefu. Benitez mwenyewe anahitaji sifa kubwa kwa hilo kwa vile alivyowapanga na kukipa motisha kikosi chake .

Umekuwa msimu mgumu kwa Newcastle lakini wana mkufunzi mzuri bila shaka.

Nadhani anafanya kazi nzuri na kwamba mashabiki wengi wanamuunga mkono na wanajua kitu anachopitia .

Sikushangazwa wakati klabu hii ilipovuka dirisha la uhamisho bila mchezaji yeyote. Kwa sababu ya kilichokuwa kikiendelea na nilijua kwamba Benitez alitaka kukiimarisha kikosi chake.

Lakini wachezaji wawili waliosajiliwa kati ya watatu Kennedy na Dubrovska wamekuwa wazuri sana na natumai Islam Slimani ataonyesha mchezo mzuri katika safu ya mashambulio wakati atakapokuwa tayari kuchezeshwa.

Newcastle inahitaji magoli ili kusonga mbele.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Ni timu gani itakayoshushwa daraja West Brom, Stoke na Huddersfield au Crystal Palace

Imekuwa wazi msimu wote kwamba Newcastle imekuwa ikihitaji nguvu mpya na ijapokuwa walifanikiwa dhidi ya Manchester United , bao moja halitasaidia kupata ushindi kila wiki.

Halikutosha dhidi ya Burnley katika mechi ya awali wakati Newcastle ilipotengeza nafasi chungu nzima na kukosa penalti kabla ya uongozi wao kukatizwa katika dakika za mwisho.

Sababu waliweza kuzuia na kuendelea ilikuwa motisha yao lakini watalazimika kufunga mabao zaidi ili kuweza kupanda juu.

Ulikuwa ushindi mzuri lakini Newcastle bado imesalia chini ya jedwali na kuna kazi ya ziada kufanyika.

Alan Shearer was speaking to BBC Sport's Chris Bevan.

Mada zinazohusiana