Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 13.02.2018

Gareth Bale
Maelezo ya picha,

Gareth Bale

Ajenti wa mshambuljia wa Real Madrid Gareth Bale anasema mchezaji huo wa Wales anapenda klabu hiyo na hataki kukihama licha ya madai kuwa Manchester United watajaribu kumsaini msimu ujao. (Tuttosport, via Manchester Evening News)

Meneja wa Manchesetr United Jose Mourinho anatajari kuboresha safu yake ya ulinzi msimu ujao huku walinzi Chris Smalling, 28, na Phil Jones, 25, wakitarajiwa kuuzwa (Mirror)

Maelezo ya picha,

Jurgen Klopp

Matumaini ya Manchester United ya kumsaini kiungo wa kati raia wa Chile Arturo Vidal, kutoka Bayern Munich ni madogo, huku mchezaji huyo wa miaka 30 bado akitaka kuchezea klabu hiyo ya Ujerumani. (Sport1, via Mirror

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ametilia shaka zaidi hatma ya Simon Mignolet huko Anfield akisema kuwa kipa huyo mbelgiji wa umri wa miaka 29, hatachaguliwa katika mechi ya Champions Ligi dhidi ya Porto siku ya Jumatano. (Guardian)

Maelezo ya picha,

Michy Batshuayi

Borussia Dortmund watajaribu kumsaini mshambuliajia wa Chelsea raia wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 24, katika mkataba wa kudumu msimu huu. (Evening Standard)

Mlinzi wa Aston Villa John Terry, 37, atafanya uamuzi kuhusu siku za usoni mwezini ya msimu huu. (Telegraph)

Maelezo ya picha,

John Terry

Leeds United watafufua jitihada zao ya kumsaini mshambuliaji wa Capri raia wa Nigeria mwenye miaka 25 Jerry Mbakogu mwishoni mwa msimu. (Mail)

Kiungo wa kati wa Juventus na Bosnia Miralem Pjanic, 27, amefichua kuwa alikataa fursa ya kujiunga na Arsenal na Tottenham hapo awali.

Uhusiano katika ya mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld na meneja Mauricio Pochettino sio mzuri baada ya mbelgiji huyo kutojumuishwa katika kikosi cha Tottenham kilichoshiriki katika mechi ya ligi ya Champions League. (Evening Standard)

Maelezo ya picha,

Sam Allardyce

Meneja wa Everton Sam Allardyce atampa fursa zaidi ya kucheza mshambuliaji raia wa Uturuki wakati timu hiyo itakuwa imejishindia nafasi katika Premier League safety. (Liverpool Echo)

Meneja wa West Ham David Moyes amekana madai kuwa ataondoka klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Talksport)

Mliki wa Stoke Peter Peter Coates amemuambia meneja Paul Lambert kuwa wachezaji wa klabu hiyo wako sawa kabisa kukiweka katika Premier League. (Stoke Sentinel)