Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 14.02.2018

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jack Butland

Manchester United wanamuangalia mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld. Mbelgiji huyo wa miaka 28 hajakuwa na mkataba kwa miezi 18 na hakujumuishwa katika kikosi cha Spurs dhidi ya Juventus katika Champions League. (Manchester Evening News)

Kipa wa England Jack Butland, 24, anasema hajaomba kuondoka Stoke baada ya kuhusishwa na kuhama kwenda Liverpool au Arsenal. (ESPN)

AC Milan wanapanga kutumia pauni milioni 30 kumtafuta kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera 28. (Tuttosport)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ander Herrera

Real Madrid wana uhakika wa kumsaini mshambuliaji wa PSG Neymar, 22, msimu huu. (Independent)

Hata hivyo waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amesema kuwa hangependa kumuua Neymar huko Madrid. (AS)

Real Madrid wana mpango wa kutumia karibu Euro milioni 600 katika kuboresha kikosi chake msimu huku wakiwa wanamlenga mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane. (Sports Illustrated)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Harry Kane

Arsenal tayari wako na mpango iwapo meneja Arsene Wenger ataondoka msimu huu. Klabu hiyo inataka kuepuka sintofahamu iliyokipata kuhusu hali ya Wenger iliyowapata mwishoni wa msimu uliopita. (Mail)

Mchezaji anayetafutwa na Chelsea Arturo Vidal anasema yuko sawa kusalia Bayern Munich. Mkataba wa kiungo huyo wa kati raia wa Chile utakamilika mwaka 2019. (Sport - in German)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wenger

Manchester City watamtaka kipa raia wa Brazil Ederson, 24, mkataba mpya miezi saba baada ya kujiunga na Premier League . (Sun)

Newcastle wana nia ya kumsaina kipa Martin Dubravka kwa mkataba kudumu. (Mirror)

Roma wanalenga kuweka malipo wa euro milioni 90 kumuachia kipa Alisson. Mchezaji huyo wa miaka 25 raia wa Brazil amehusishwa na kuhama kwenda Liverppool. (Calciomercato)

Haki miliki ya picha PA
Image caption Victor Anicheb

Bolton wanammezea mate mshambuliaji wa zamani wa West Brom Victor Anichebe. Mnigeria huyo wa miaka 29 hana mkataka baada ya kucheza katika Super League ya China. (Birmingham Mail)

Kiungo wa zamani wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan, 29, anasema alichagua muda bora kuondoka klabu ili kufufua upya taaluma yake huko Arsenal. (London Evening Standard)