Liverpool yailima FC Porto 5-0

Sadio Mane
Maelezo ya picha,

Sadio Mane amefunga mabao sita katika Champions League msimu huu

Sadio Mane walifunga hat-trick wakati Liverpool walipata ushindi mkubwa kwa kuwalima FC Porto 5-0

Sadio Mane alikuwa wa kwanza kutikiza wafu wa kipa Jose Sa.

Mohamed Salah akafuatia na bao la pili na lake la 31 tangu ajiunga na Liverpool

Maelezo ya picha,

Liverpool wako katika awamu ya maondoano katika Champions League kwa mara ya kwanza katika miaka saba

Mashambulizi ya counter-attack ya Liverpool yalisababisha Sa kuutema mkwaju kutokana na shambulizi lililofanywa na Mane baada ya kupata mpira safi kutoka kwa Roberto Firmino kabla ya Firmino kufunga bao lake la 21 kwenye msimu.

Maelezo ya picha,

Salah amefunga mabao 30 kwa mechi 37 akiichezea Liverpool msimu huu

Porto imepoteza mechi mbili tu katika mashindano yote kabla ya mechi ya Jumatano lakini wakati huu ilishindwa kustahimili kishindo cha Liverpol kutoka kwa washambuliaji walionolewa.

Maelezo ya picha,

Sadio Mane ndiye mchezaji wa nne wa Liverpool kufungua kwa hat-trick katika Champions League, baada ya Michael Owen, Yossi Benayoun na Philippe Coutinho