Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 15.02.2018

Mauricio Pochettino Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mauricio Pochettino

Tottenham wana nia ya kumpa meneja Mauricio Pochettino mkataba mpya wa pesa nyingi. Raia huyo wa Argentina aliweka sahihi mkataba mpa ya miaka mitano mwaka 2016 wa pauni milioni 5.5 kwa mwaka. (Telegraph)

Real Madrid wanaongoza mbio za kumwinda mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld. Manchester City, Chelsea na Manchester United pia nao wanamwinda mbelgiji huyo wa miaka 28. (Mirror)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marouane Fellaini

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini amekubali kujiunga na Besiktas mwisho wa msimu. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, 30, utakamilika mwisho wa msimu. (Fotomac - in Turkish)

Jeventus wameuliza kuhusu kiungo wa kati wa Liverpool Jack Wilshere ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu. (Mirror)

Everton na Tottenham wote wanamzea mate wing'a wa PSV Steven Bergwijn. Mchezaji huyo wa miaka 20 aliiwakilisha uholanzi katika kwenye kikosi cha chini ya miaka 17 na 21. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Erik Lamela

Kiungo wa kati wa Tottenham Erik Lamela anaeleza kuhama kwake kwenda Inter Milan. Muargentina huyo amerejea tu baada ya jeraha lililomweka nje kwa zaidi ya mwaka mmoja. (Talksport)

Arsenal na Chelsea wote wanafuatilia mkataba wa mlinzi Luke Shaw wa Manchester United. Jose Mourinho amethibitisha kuwa mlinzi huyo yuko katika mkondo wa mkataba mpya lakini mazungumzo bado hayajaanza. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba

Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Ufaransa Paul Pogba, 24, anataka meneja Jose Mourinho kubadili mfumo ya kikosi ili apate kushiriki katika safu ya mshambuliaji (Daily Record)

Meneja wa Stoke Paul Lambert anasema kuwa kipa Jack Butland, 24, hataathiriwa na uvumi kuhusu hatma yake (Stoke Sentinel)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Gabriel Jesus

Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, 20, ametafuta usaidizi wa mBrazil mwenzake baada ya kuchukua muda mrefu kupona jeraha. Wote hao walikutana katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Neymar wiki iliyopita. (Daily Mail)

Everton wamemsadia shabiki wa miaka 100 kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kumualika kwenye mazoezi yao pamoja na kikombe cha chai na mshambuliaji wa zamani wa Everton Duncan Ferguson. (Liverpool Echo)

Mada zinazohusiana