Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 16.02.2018

Paul Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid inamuwania mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Paul Pogba msimu huu wa joto, lakini watahitaji kutoa zaidi ya £ milioni 120 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ndiye mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili alipohamia Old Trafford. (Sun)

Lakini Pogba ana uwajibikaji kuondosha tofuati zozote za kimaono na meneja wa United Jose Mourinho. (Telegraph)

Jitihada za Pogba akiwa ndani ya Manchester United zimepungua baada ya kuwasili kwa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Chile Alexis Sanchez, mwenye mri wa miaka 29, kutoka Arsenal, kwa mujibu wa aliyekuwa kapteni wa timu hiyo ya mashetani wekundu Paul Ince. (Mirror)

Mke na mwakilishi wa kapteni wa Inter Milan Icardi, anafanya mazungumzo kujaribu kufikia makubaliano na Manchester United, licha ya mchezaji huyo kuhusishwa na uhamisho wa msimu wa joto kwenda Real Madrid. (Corriere dello Sport via ESPN)

Liverpool inajaribu kufikia makubaliano kumsajili kipa wa Roma Alisson, mwenye umri wa miaka 26, kabla ya kufunguliwa dirisha la uhamisho katika msimu wa joto, lakini raia huyowa Brazil ana thamani ya £milioni 62 na wanakabiliwana ushindani mkubwa wa kutaka kumsajili. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Joe Hart (kushoto)

Kwa upande mwingine huenda Liverpool ikawacha kumuwania Alisson na kusalia na kipa wa Ujerumani Loris Karius. (Telegraph)

Kipa wa England Joe Hart, mwenye umri wa miaka 30, yuko tayari kujiuzulu Manchester City na ahamie ng'ambo msimu huu wa joto baada ya kutemwa akiwa katika mkopo huko West Ham msimu huu. (Sun)

Malcom, mchezaji wa kiungo cha mbele wa Brazil anayelengwa na Arsenal na Tottenham, amethibitisha ana makubaliano na klabu aliyopo sasa ya Bordeaux yanayomruhusu kuondoka msimu huu wa joto. (UOL via Sky Sports)

Aliyekuwa kapteni wa England John Terry anataka kurudi Chelsea katika jukumu la kuwa kocha anapopanga njia yakurudi katika kazi hiyo kuu huko Stamford Bridge. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 anayecheza kiungo mlinzi anamaliza mkataba wake na Aston Villa mwezi July wakati mkataba wake wa mwaka unapomalizika. (Mirror)

Huenda Tottenham ikafikiria ombi kwa mlinzi wa kimataifa raia wa Ubelgiji Toby Alderweireld, mwenye umri wa miaka 28, msimu huu wa joto lakini wana imani kuwa wataendelea kuwahifadhi wachezaji wote wanaowataka wasalie. (London Evening Standard)

Mazungumzo ya hivi karibuni ya Spurs na mlinzi huyo kutafuta mkataba yaliishia bila maafikiano. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Thorgan Hazard

Leicester City wanamuwania mchezaji wa kiungo cha kati wa Borussia Monchengladbach na raia wa Belgium Thorgan Hazard,mwenye umri wa miaka 24, kakake mchezaji wa Chelsea Eden. (HLN - in German)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Watford Richarlison, bado hajaondosha matumaini ya kuhamia Chelsea katika msimu ujao wa joto. The Blues wanafikiria ombi la kumwania mchezaji huyo timu ya taifa ya Brazil ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 20 lakini huenda wakakabiliwana ushindani kutoka Arsenal naTottenham. (London Evening Standard)

Mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos anasema Zinedine Zidane huenda bado akaondoka Bernabeu mwishoni mwa msimu hata iwapo atashinda taji. (Express)

Nyota wa Barcelona Lionel Messi, mwenye umri wa miaka 30, anatarajiwa kupumzishwa zaidi katika kipndi kilichosalia cha msimu katika jitihada za kuimarisha uchezajiw a timu ya Argentina katika michuano muhimu. (Marca)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Nyota wa Barcelona Lionel Messi

Aston Villa imefanya mazungumzo mazuri na wamiliki wakuu wa klabu ya Denmark Lyngby Boldklub kuhusu uwezekano wa kufikia ushirikiano. (Birmingham Mail)

Bingwa wa Uholanzi Patrick Kluivert amemshauri mtoto wake Justin Kluivert, mwenye umri wa miaka 18, anayeichezea Ajax, akatae kuhamia katika ligi ya England na badala yake afikirie kucheza katika ligi ya Uhispania. (Metro)

Wake wa wachezaji wa Argentina Angel di Maria, mwenye umri wa miaka 30, na beki wa Brazil Thiago Silva, mwenye umri wa miaka 33, wamemshutumu meneja wa Paris St-Germain - Unai Emery baaday a wachezaji hao wawili kutemwa baada ya kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid. (Marca)