Waafrika wanaopigania ndoto zao katika Olimpiki

Mkenya Sabrina Simader

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mkenya Sabrina Simader

Huenda hakuna Waafrika wengi wanaoshindana katika mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi huko Pyeongchang, Korea kusini.

Lakini kwa wachache walioko huko wanajizatiti kuonyesha umahiri wao.

Mkenya Sabrina Simader, raia wa Madagascar Mialitiana Clerc na Mathilde-Amivi Petitjean raia wa Togo walikwea milima kupigania ndoto zao za Olimpiki.

Kwa bahati mbaya, matokeo hayajakuwa mazuri vile.

Mathilde-Amivi Petitjean wa Togo aliibuka nambari 83 kati ya 90 katika mashindano ya kilomita kumi kuteleza kwenye barafu dakika 7.34 nyuma ya mshindi wa nishani ya dhahabu Ragnhild Haga wa kutoka Norway.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mialitiana Clerc wa Madagascar

Mialitiana Clerc kutoka Madagascar aliibuka katika nafasi ya 48 kati ya 58 takriban sekundi 19 nyuma ya Mmarekani Mikaela Shiffrin, aliyeshinda dhahabu.

Huku naye Mkenya Sabrina Simader alishindwa kumaliza awamu yake ya pili ya mashindano hayo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mathilde-Amivi Petitjean wa Togo

Hii leo mashabiki wa mashindano hayo ya Olimpiki watamtizama Samir Azzimani wa Morocco katika mashindano ya wanaume ya kilomita 15 mtindo wa wazi wa kuteleza kwenye barafu.

Akwasi Frimpong wa Ghana anatarajia kujiimarisha katika nafasi yake - ya mwisho - katika shindano la skeleton.

Nigeria inashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo ya Olimpiki ya msimu wa barafu wakati Simidele Adeagbo akishiriki kwa upande wa wanawake wa mashindano ya skeleton.