Jose Mourinho: Sina ugomvi na Pogba na haondoki ng'o

Jose Mourinho na kiungo wa kati Paul Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho na kiungo wa kati Paul Pogba

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa ripoti kwamba kiungo wa kati wa klabu hiyo anajuta kujiunga na Man United na kwamba huenda angeondoka mwisho wa msimu huu ni za uongo.

Pogba alidaiwa kukasirishwa na hatua ya Mourinho kumchezesha katika safu isio ya mashambulio , lakini Mourinho amesema kuwa hilo sio kweli.

Vilevile amewakosoa wachanganuzi wa soka akisema kuwa sio muhimu kutaja kuhusu mazungumzo yao na wachezaji.

Lakini ameongezea kuwa Pogba anakubali kwamba hajakuwa akicheza vyema.

Alipoulizwa fikira zake kuhusu uvumi huo katika vyombo vya habari, Mourinho alijibu, nadhani una maneno matamu kwa sababu ukisemu uvumi mwingi unafaa kuongezea uongo mwingi.

''Usiwe mzuri sema ni uongo.Ni uongo mkubwa sana kwamba uhusiano wetu sio mzuri, ni uongo kwamba hatuwasiliani, uongo kwamba hatukubaliani na eneo lake analofaa kucheza.Ni rahisi na ukweli kwamba Paul hakucheza vyema dhidi ya Newcastle lakini watu wengine hulipwa mamilioni, usikubali watu kusoma vitu ambavyo sio vya kweli.Ni tatizo langu na la Paul kuimarisha kiwango chake cha mchezo, haufai kudanganya''.