Giroud aifungia Chelsea bao lake la kwanza tangu uhamisho wake

Olivier Giroud ampiga busu katika paji la uso Emmerson baada ya mchezaji huyo kumpigia pasi murua iliomfanya kufunga bao lake la kwanza akiwa Chelsea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Olivier Giroud ampiga busu katika paji la uso Emmerson baada ya mchezaji huyo kumpigia pasi murua iliomfanya kufunga bao lake la kwanza akiwa Chelsea

Olivier Giroud na Willian waliisaidia timu ya Chelsea kuicharaza Hull City mabao manne na hivyobasi kufika katika robo fainali ya kombe la FA na sasa Mkufunzi wa klabu hiyo Antonio Conte anasema kuwa wamempatia sababu njema kuhusu mechi kati ya timu hiyo na Barcelona.

Willian alionyesha mchezo mzuri katika mechi yote na alifunga bao la kwanza kwa kuupinda mpira katika kona ya goli akiwa nje ya eneo hatari.

Pedro alifunga bao la pili baada ya kumchenga David Marshall kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Cesc Fabregas kutoka katikati ya uwanja.

Willian alifunga bao la tatu kutoka maguu 25 baada ya kucheza nipe nikupe na Giroud .

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa baadaye alifunga bao lake la kwanza tangu uhamisho wake kutoka Arsenal akiwa karibu na goli kufuatia krosi iliopigwa na Emerson Palmieri kutoka wingi ya kushoto.

Chelsea watawajua wapinzani wao wa kombe la FA siku ya Jumamosi.

Baadye watachuana na Bercalona siku ya Jumanne katika robo fainali ya klabu bingwa Ulaya.

Conte alisema kuwa ilikuwa mechi nzuri baada ya Olivier Giroud kufunga huku Willian akionyesha mchezo mzuri.

''Kwa kweli nikienda nyumbani sasa nitakuwa na chaguo kwa kuwa wachezaji wengi wamethibitisha kwamba viwango vya vya mchezo wao viko juu

Mada zinazohusiana