Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 17.02.2018

Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 21
Image caption Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 21

Arsenal ndio klabu ya hivi karibu ambayo inamnyatia mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 21. Raia huyo wa Ujerumani ambaye pia anasakwa na Chelsea, Liverpool na Manchester United ana thamani ya £50m na amekataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Bundesliga. (Sun)

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amemuorodhesha kiungo wa kati wa Lyon Nabil Fekir kuwa mchezaji anayemtaka sana .Wenger yuko tayari kutoa dau la £45m ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24- (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Tottenham Victor Wanyama

Liverpool inamtazama kiungo wa kati wa Tottenham na Mkenya Victor Wanyama mwenye umri wa miaka 26 kufuatia madai kwamba huenda kiungo wa kati wa Ujerumani Emre Can akaondoka Anfield. (Mail)

Wadhfa wa mkufunzi wa West Brom Alan Pardew upo hatarini kufuatia hatua ya wachezaji wanne kuomba msamaha baada ya kuiba gari la teksi nje ya mgahawa mmoja nchini Barcelona siku ya Alhamisi. (Sun)

Image caption Pep Guardiola

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa klabu hiyo haikufanya makosa yoyote katika jaibio lao lililofeli la kujaribu kumsajili winga wa Leicester Riyad Mahrez.. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 24, halengwi na Real Madrid . (Sky Sports)

Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Nice na Ivory Coast mwenye umri wa miaka 26 Jean Michael Seri, ambaye atawachiliwa na timu yake iwapo mnunuzi atalipa £33m. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michy Batshuayi,

Mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, ambaye yuko klabu ya Dortmund kwa mkopo anasema kuwa hakuwa na muda mzuri katika klabu ya Chelsea lakini sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anahisi kuaminiwa na klabu hiyo mpya. (Sporza, via Mirror)

Mshambulaji wa Uhispania Sandro Ramirez, 22, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Sevilla ameiambia Everton kwamba hataki kurudi.(Mirror)

Image caption Andres Iniesta

Nahodha wa klabu ya Barcelona Andres Iniesta, 33, huenda akaondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo ametakiwa kujiunga na klabu ya China ya Tianjin Quanjian kwa dau la £31m- kwa msimu(Diario Sport - in Spanish)

Crystal Palace wanataka kumsajili kipa wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 35 Diego Cavalieri, ambaye anapatikana kwa uhamisho huru. Mkufunzi wa klabu hiyo Roy Hodgson anahitaji kipa wa ziada wa kuziba pengo la Wayne Hennessey kwa kuwa Julian Speroni anauguza jeraha.(Evening Standard)

Image caption Romelu Lukaku

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, 24, anapanga kurudi Ubelgiji kwa klabu yake ya utotoni Anderlecht wakati atakapoondoka Manchester United. (HLN, via Manchester Evening News)

Kiungi wa kati wa zamani wa Leicester City Ethan Hodby, 19, ameanza kutafuta klabu mpya kwa kutangaza uwepo wake katika mtandao waLinkedIn. (Metro)

Babake Neymar amewashutumu wakosoaji wa mwanawe katika mechi ambapo Paris St-Germain ilishindwa na Real Madrid (Express)

Mada zinazohusiana