Real Madrid yailaza Real Betis 5-3

Wachezaji wa klabu ya Real Madrid Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa klabu ya Real Madrid

Marco Asensio alifunga mabao mawili na kuisaidia Real Madrid kuizaba klabu ya Real Betis 5-3 na kuipatia klabu hiyo ushindi wa tatu mfululizo.

Kikosi cha Zinedine Zidane kilichukua uongozi wakati Asensio alipofunga lakini Betis ikisawazisha kupitia Aissa Mandi.

Bao la kujifunga mwenyewe la Nacho liliiweka Betis kifua mbele katika kipindi cha kwanza lakini Sergio Ramos , Asensio na Cristiano Ronaldo walifunga na kuwaweka mabingwa hao watetezi kifua mbele .

Bao la Sergio Leons la dakika za lala salama liliitia wasiwasi Real Madrid kabla mchezaji wa ziada Karim Benzema kucheka na wavu na kufanya mambo kuwa 5-3.

Kulikuwa na hari kubwa kuhusu mchezo ulioonyeshwa na Madrid.

Bao la tatu na la nne yaliofungwa na Asensio na Ronaldo yalikuwa bora. Real Madrid ambayo ipo katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 17 nyuma ya viongozi wa ligi Barcelona, ambao waliishinda Eibar 2-0 siku ya jumamosi.

Kikosi hivcho cha Zidane kiko pointi 10 nyuma Real Mdrid na pointi moja nyuma ya Valencia iliopo nafasi ya tatu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii