Kenya yamsaka kocha mpya wa Harambee Stars baada ya Paul Put kujiuzulu

Kenya inamsaka mkufunzi mpya wa timu yake ya taifa baada ya kocha Paul Put kujiuzulu miezi mitatu baada ya kuzinduliwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kenya inamsaka mkufunzi mpya wa timu yake ya taifa baada ya kocha Paul Put kujiuzulu miezi mitatu baada ya kuzinduliwa.

Kenya inamsaka mkufunzi mpya wa timu yake ya taifa baada ya kocha Paul Put kujiuzulu miezi mitatu baada ya kuzinduliwa.

Hii ilithibitishwa Jumatatu jioni na taarifa iliotolewa na shirikisho la soka nchini humo FKF kupitia meneja wa mawasiliano na uhusiano mwema Barry Otieno ambaye alielezea kwamba mkufunzi huyo alijiuzulu kutokana na matatizo ya kibinafsi huku Stanley Okumbi akichukua mahala pake kwa muda.

''Shirikisho la soka la Football Kenya lingependa kuwaambia mashabiki wa soka nchini Kenya kwamba bwana Pual Put amejiuzulu rasmi kama mkufunzi wa timu ya taifa kutokana na maswala ya kibinafsi.

''Hatahivyo kujiuzulu kwa kocha huyo ni pigo katika harakati za timu ya taifa kuelekea katika kufuzu mashindano ya AFCON 2019 kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu cha timu''.

Na kufuatia hatua hiyo FKF imeanza mchakato wa kutafuta suluhu ya kujaza wadhfa wa Put huku Stanley Okumbi akichukua mahala pake kwa muda.

''Mwisho FKF inamshukuru bwana Put kwa huduma zake wakati akiwa mkufunzi mkuu wa Harambee Stars mbali na kumtakia mema katika kazi yake siku zijazo'', taarifa hiyo ilisema.