Meneja wa Chelsea Antonio Conte: Tutailaza Barcelona mechi ya marudio Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA

Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu

Mkufunzi Antonio Conte amesema kuwa Chelsea "itajaribu kufanya kitu cha kipekee'' na kuitoa Barcelona katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya sare 1-1 katika awamu ya kwanza.

Willian aliiweka kifua mbele The Blues lakini Lionel Messi alisawazisha dakika 15 kabla ya mechi kukamilika baada ya makosa ya Andreas Christensen katika mechi ya kufuzu katika robo fainali ya kombe hilo.

Barcelona ambayo iko pointi saba mbele kileleni La Liga haikutekeleza mashambulizi yoyote makali hadi waliposawazisha.

''Tulikuwa tunakaribia kuwafunga," alisema mkufunzi huyo wa Chelsea. ''Tulifanya kosa moja, ni aibu na tumevunjwa moyo na matokeo''.

Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje ya eneo la hatari kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu kupitia shambulio alilotekeleza akiwa maguu 20.

Hatahivyo dakika 13 baadaye, Christensen alifanya makosa kwa kutoa pasi mbaya iliochukuliwa na Andres Iniesta aliyeshirikiana na Messi ambaye alifunga bao lake la kwanza la vilabu bingwa dhidi ya klabu hiyo ya London.

Christensen mwenye umri wa miaka 21 alikuwa ameichezea Chelsea mara tatu pekee kabla ya msimu huu lakini ameshirikishwa sana msimu huu huku beki wa kati Gary Cahill akipumzishwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Christensen mwenye umri wa miaka 21 alikuwa ameichezea Chelsea mara tatu pekee kabla ya msimu huu

Hata hivyo Conte alimtetea beki huyo wa Denmark licha ya makosa yake yalioipatia Barca bao muhimu la ugenini huku awamu ya pili ya mechi ya marudiano ikichezwa tarehe 14 mwezi Machi nchini Uhispania.

''Tulicheza vizuri sana," alisema raia huyo wa Italia.

''Tunazungumzia kuhusu mchezaji mdogo sana. Ni vyema kwamba anaweza kucheza katika mechi kama hii akionekana mchezaji aliyekomaa.

Alikuwa miongoni mwa wachezaji wazuri sana usiku huu. Ni vigumu kumtaja mchezaji mmoja lakini nadhani Christensen alicheza mechi kubwa na nilifurahishwa na mchezo wake. Tulifanya kosa moja lakini tunajua ukicheza na wapinzani kama Messi, Iniesta na Suarez unapofanya makosa unagharamika."

Nini kitafuata?

Chelsea watacheza mechi tatu kabla ya kukutana na Barcelona kwa mechi ya marudiano, mechi hizo zikijumuisha mechi za ugenini Ligi ya Premia dhidi ya klabu mbili za Manchester.

Watakutana na Manchester United Jumapili, 25 Februari (14:05 GMT) na kisha wakutane na Manchester City Jumapili itakayofuata (16:00 GMT).

Barcelona watarejea uwanjani La Liga Jumamosi, 24 Februari kwa mechi ya nyumbani dhidi ya klabu ya Girona ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya nane.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii