Tetesi za soka Ulaya Jumatano 21.02.2018

Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Christian Pulisic
Image caption Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Christian Pulisic

Chelsea inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Bayern Munich katika kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Christian Pulisic. (Mail)

West Ham iko tayari kumpatia David Moyes mkataba wa miaka miwili mwisho wa msimu huu iwapo atawasaidia The Hammers katika ligi ya Uingereza na raia huyo wa Uskochi tayari anatafuta wachezaji wa kuwasajili msimu ujao(Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa Lazio na Uholanzi Stefan de Vrij , 26 yuko tayari kuondoka katika klabu yake na kuelekea Manchester United

Beki wa Lazio na Uholanzi Stefan de Vrij , 26 yuko tayari kuondoka katika klabu yake na kuelekea Manchester United lakini Everton na Arsenal pia wana hamu ya kumsajili(Mirror).

United pia ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Lazio na raia wa Itali Jorginho, 26. (sun) Barcelona imeishinda Manchester United katika kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Gremio mwenye umri wa miaka 21 Arthur (mail).

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucore

Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucore ,25, amedai kwamba klabu kubwa za ligi ya Uingereza zinamnyatia huku Arsenal ikiwa ndio lengo lake kubwa kujiunga nayo.(Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Watford Marco Silva ndio anayepigiwa upatu kumrithi Alan Pardew iwapo atandoka West Brom(Birmingham Mail)

Image caption Crystal Palace imejiandaa kumsaini kipa wa zamani wa Liverpool na Brazil Diego Cavalieri katika uhamisho wa bure(ESPN)

Crystal Palace imejiandaa kumsaini kipa wa zamani wa Liverpool na Brazil Diego Cavalieri katika uhamisho wa bure(ESPN)

Liverpool inajiandaa kumsajili kinda wa Lyon na Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Mohamed Bahlouli. (France Football via Sun)

Lengo la kocha Jurgen Klopp la kumsajili kipa wa Roma Alisson imepigwa jeki baada ya klabu hiyo ya Itali kupata kipa atakayechukua mahala pake (Gianluca di Marzio via Sun)

Image caption Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand

Rio Ferdinand haamini kwamba mkufunzi wa Chelsea atakuwa na wasiwasi katika kutete awadhfa wake katika klabu hiyo ya Stamford Bridge licha ya timu hiyo kuwa pinti 19 nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City. (BT Sport via Star)

Afisa anayesaka wachezaji katika klabu ya Chelsea Eddie Newton amefichua kwamba amemkagua mshambuliaji wa Everton na Uturuki Cenk Tosun, 26, na anamtarajia kufanya vyema katika klabu hiyo. (Liverpool Echo)

Philippe Coutinho alikuwa na wakati mgumu katika kipindi cha saa 24 zilizopita mjini Barcelona baada ya gari lake kuvutwa kwa kuliegesha katika eneo lisilofaa na baadaye nyumba yake ikavunjwa na kuibiwa. (Daily Mail)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii