Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 22.02.2018

pogba
Maelezo ya picha,

Pogba

Ajenti wa kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba amewasilisha ombi la kuhama la mchezaji huyo katika klabu kubwa za Ulaya .

Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 alianza mechi ya United ya 0-0 dhidi ya Sevilla siku ya Jumatano akicheza kama mchezaji wa ziada. (Sports Illustrated)

Maelezo ya picha,

kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, 25

Real Madrid inamtaka kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, 25, kuchelewesha kutia saini kandarasi yake mpya na klabu hiyo hadi mwezi Aprili ambapo watafanya uamuzi wa kumsajili raia huyo wa Ubelgiji ama kipa wa Man United David de Gea, 27. (Telegraph)

Courtois amekiri kwamba ajenti wake atasikiliza ombi kutoka timu hiyo ya La Liga.. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Beki wa Uingereza Harry Maguire

Beki wa Uingereza Harry Maguire, 24, yuko tayari kumaliza soka yake katika klabu ya leicester , licha ya beki huyo anayedaiwa kuwa na thamani ya £50m kuhusishwa na uhamisho wa klabu ya Manchester City. (Sun)

Manchester United ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Dinamo Zagreb mwenye umri wa miaka 19 Nikola Moro, ambaye ametajwa kuwa 'Luka Modric mpya' (Talksport)

Maelezo ya picha,

Claudio Ranieri

Klabu ya ligi ya kwanza ya Nantes nchini Ufaransa imesema kuwa haitamzuia meneja wake Claudio Ranieri iwapo atapewa wadhfa wa kocha mkuu wa Itali. (L'Equipe - in French)

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, 30, ananyatiwa na klabu nne za Ufaransa ikiwemo Lyon, Paris St-Germain lakini mchezaji huyo hapendelei kuondoka. (AS)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Beki wa Tottenham Davinson Sanchez,

Beki wa Tottenham Davinson Sanchez, 21, anasema kuwa hapendelei uhamisho wa kuelekea Real Madrid mwisho wa msimu huu .Raia huyo wa Colombia alijiunga na Spurs kutoka Ajax Agosti iliopita. (Mirror)

West Bromwich Albion inamchunguza meneja wa klabu ya Ostersunds Graham Potter. Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 42 anasema kuwa anapanga kufunza katika ligi ya Uingereza katika siku za usoni. (Daily Mail)

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anamtaka mshambuliaji wa Uingereza Danny Welbeck, 27, kutia saini kandarasi mpya na Arsenal . (Daily Mail)

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anamtaka mshambuliaji wa Uingereza Danny Welbeck, 27, kutia saini kandarasi mpya na Arsenal . (Daily Mail)

Mchezaji wa zamani wa Newcastle na Tottenham David Ginola amepata mtoto mwengine akiwa na umri wa miaka 51 miaka miwili baada ya kupata mshutuko wa moyo wakati wa mechi ya hisani. (BirminghamLive)