Mitchy Batshuayi apigiwa kelele za tumbili

Mitchy Batshuayi anasema kuwa alisikia kelele za tumbili katika eneo la mashabiki wakati ambapo Borussia Dortmund ilikuwa ikiishinda klabu ya Atalanta katika ligi ya Yuropa huko Bergamo
Image caption Mitchy Batshuayi anasema kuwa alisikia kelele za tumbili katika eneo la mashabiki wakati ambapo Borussia Dortmund ilikuwa ikiishinda klabu ya Atalanta katika ligi ya Yuropa huko Bergamo

Mitchy Batshuayi anasema kuwa alisikia kelele za tumbili katika eneo la mashabiki wakati ambapo Borussia Dortmund ilikuwa ikiishinda klabu ya Atalanta katika ligi ya Yuropa huko Bergamo.

Mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye anaichezea Dortmund kwa mkopo alituma ujumbe katika mtandao wa twitter akisema: huu ni mwaka 201`8 na bado kuna kelele za sauti ya tumbili katika eneo la mashabiki....siamini.

''Natumai mulifurahia kutazama mechi za ligi ya Yuropa katika runinga''.

Dortmund ilishinda 4-3 kwa jumla baada ya marcel Schmelzer kusawazisha bao lililofungwa na Wataliano hao.

Mwezi uliopita , Atalanta ilipigwa marufuku ya kutocheza mechi moja baada ya beki wa Napoli kalidou Koulibaly kupigiwa kelele cha tumbili wakati wa mechi ya ligi ya Serie A.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii