Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 23.02.2018

Kipa wa Manchester United David De Gea
Maelezo ya picha,

Kipa wa Manchester United David De Gea

Kipa wa Spain David de Gea, 27, anatarajiwa kuandikisha kandarasi mpya na klabu ya Manchester United akiipuzilia mbali uhamisho wake kuelekea Real Madrid. (Times - subscription)

Real Madrid inamchunguza winga wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambaye hajaanza mazungumzo rasmi ya kuongeza kandarasi mpya na klabu yake .Mkataba wa raia huyo wa Uingereza unakamilika 2020. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anahisi kwamba kocha Mourino anambagua na kwamba anataka kuthaminiwa tena (Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anahisi kwamba kocha Mourino anambagua na kwamba anataka kuthaminiwa tena (Mail)

Mourinho alimwambia raia huyo wa Ufaransa 'kuona ishara za kuondoka' katika klabu hiyo baada ya mkutano wa baada ya mazoezi (Sun)

Maelezo ya picha,

Gareth Bale

Maafisa wakuu katika klabu ya Real Madrid wamekiri kwa faragha kwamba wako tayari kumuachilia mshambuliaji wa Wales Gareth Bale kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu huu.(Independent)

Chelsea inamchunguza nahodha wa Newcastle Jamaal Lascelles, 24, na huenda ikamnunua beki huyo mwisho wa msimu huu.. (Evening Standard)

Maelezo ya picha,

Gareth Darmian

Juventus wameafikiana makubaliano ya kumsajili beki wa Manchester United Matteo Darmian, 28, mwisho wa msimu huu. (Calciomercato - in Italian)

Babake mshambuliaji wa PSG Neymar aliendelea kuwasiliana na rais wa Real Madrid Florentino Perez huku akijaribu nyote huyo kujiunga na klabu hiyo. (Diario Gol via Star)

Maelezo ya picha,

Neymar

kiungo wa kati wa zamani wa Sunderland Jan Kirchhoff, 27, yuko katika mazungumzo ya kujiunga na klabu ya ligi ya kwanza Bolton hadi mwisho wa msimu huu . (Sky Sports)

Klabu ya China ya Dalian Yifang inakaribia kumsajili beki wa West Ham Jose Fonte, 34, kwa dau la £5m. Raia huyo wa Ureno hahitajiki tena na kocha David Moyes. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco,

Winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 24, anatarajiwa kuondoka Atletico Madrid na kujiunga na klabu ya Dalian Yifang kwa dau la Yuro30m (£27m). Mkataba unaweza kuafikiwa mwisho wa wiki hii. (Marca)

Barcelona wameamua kutomfuatilia nahodha wa Lyon Nabil Fekir. Arsenal wamehusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo utakaogharimu dau la £45m . (sport)

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kuleta 'utulivu' kati yake na mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte wakati timu hizo mbili zitakapokutana siku ya Jumapili.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mourinho na Conte

Mourinho alisema Januari kwamba hatopigwa marufuku kwa match-fixing", Conte alimjibu kwa kumuita Mourinho mtu mdogo.

(Mirror)Atletico Madrid wanamtaka beki wa West Ham Reece Oxford, 19, mbaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Bundesliga Borussia Monchengladbach. Klabu hiyo inamthamini kinda huyo kuwa na thamani ya £12m. (Telegraph)