Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 25.02.2018

Neymar

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Neymar

Mshambualiaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26, amewaambia Real Madrid kuwa anataka pesa zaidi kuliko za mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo ili aweze kuhamia Bernabeu. (Sunday Express)

Kiungo wa kati mfaransa Paul Pogba yuko tayari kuondoka Manchester United ikiwa meneja Jose Mourinho ataendelea kuwepo Old Trafford. (Sun on Sunday)

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Louis van Gaal

Manchester United ni kati ya vilabu vikuu vinavyomtazana kiungo wa kati wa Lazio raia wa Serbia, Sergej Milinkovic-Savic, ambaye ambaye thamani yake huenda ikawa pauni mioni 80. (Sunday Mirror)

Meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal, huenda akachukua mahala pake Antonio Conte, huko Chelsea ikiwa uhusiao wake na Chlesea utazorota zaidi. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

David de Gea

Kipa wa Manchester United na Uhispania David de Gea anataka mshahara wa paunia 350,000 kwa wiki ili kusalia huko Old Traford.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 27 analipwa pauni 180,000 kwa wiki laki yuko nyuma wa Mchile Alexis Sanchez, anayelipwa pauni 505,000 kwa wiki. (Sun on Sunday)

Mlinzi wa Manchester City Aymeric Laporte, 23, anasema alikuwa sawa kukataa ofa ya kwanza kutoka kwa viongozi hao wa Premier League miezi 18 iliyopita. (Sunday Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atawanyima wachezaji wake sherehe ikiwa watashinda mechi ya kombe la Carabao leo Jumapili kwa sababu anataka wawe hali nzuri kwa mechi ya Alhamsia dhihi ya Arsenal huko Emirates. (Independent on Sunday)

Chelsea na Crystal Palace wametofautiana kuhusu njia bora ya kumtendea kiungo wa kati aliye na jeraha Ruben Loftus-Cheek.

Mchezahua huo wa miaka 22 ambaye kwa mkopo huko Palace amakuwa nje tangu mwezi Disemba. (Daily Star Sunday)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez hana hofu kuhusu jereha la mshambuliaji Islam Slimani ambalo huenda likamweka nje hadi mwezi ujao. (Chronicle)