Man City washindi wa kombe la Carabao, wailaza Arsenal 3-0

Manchester City wameshinda kombe la ligi kwa mara ya tano ikiwa ni Liverpool pekee walioshinda idadi hiyo
Image caption Manchester City wameshinda kombe la ligi kwa mara ya tano ikiwa ni Liverpool pekee walioshinda idadi hiyo

Pep Guardiola ameshinda taji lake la kwanza msimu huu baada ya Manchester City kuifunga Arsenal katika fainali za kombe la Carabao mchezo uliopigwa kwenye dimba la Wembley.

Man City wameshinda kwa magoli 3-0 katika mchezo ambao City ilitawala kwa kiasi kikubwa.

Magoli ya City yamepachikwa na Sergio Aguero baada ya kupokea pasi kutoka kwa Claudio Bravo, Vincent Kompany akafunga la pili na David Silva akafunga la tatu na la ushindi.

Image caption Wachezaji wa City wakishangilia kikombe cha kwanza kwa msimu huu

City wametoa kichapo hicho baada ya kuondolewa katika kombe la FA siku ya Jumatatu walipocheza na Wigan Athletic.

Arsenal haikuonyesha makali yake, huku msambuliaji wake mpya Pierre-Emerick Aubameyang akishindwa kung'ara.

Image caption Arsenal hawakuwa na kiwango cha kuridhisha

Vincent Kompany ambaye alikosekana uwanjani kwa muda mrefu alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii