Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.02.2018

Robert Lewandowski

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Robert Lewandowski

Real Madrid wanafikiria kumwendea mshambulizi wa Bayern Munich raia wa Poland Robert Lewandowski, 29, mwisho wa msimu baada ya kuwepo ugumu wa kumsaini mshambulizi wa England Harry Kane, 24, kutoka Tottenham. . (Independent)

Everton wana mpango wa kumfuta meneja Sam Allardyce mwishoni wa msimu na meneja wa Shakhtar Paulo Fonseca anaongoza orodha ya wale watakaochukua nafasi yake. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Thibaut Courtois

Chelsea wanaratajiwa kupangua mazungumzo ya kumsaini kipa raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 25, ambaye pia analengwa na Real Madrid, hadi baada ya mechi zao kuu dhidi ya Barcelona na Leicester mwezi Machi. (London Evening Standard)

Meneja Jose Mourinho hana furaha kuhusu jinsi Manchester United inawapa mikataba mipya wachezaji wake. (Mail)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Antonio Conte

Matumaini ya Luis Enrique kuchukua mahala pake Antonio Conte kama meneja wa Chelsea yatatimia ikiwa yuko tayari kukukalia mshahara mdogo kuliko na aliolipwa huko Barcelona. (Telegraph)

Taarifa kutoka klabu ya Paris St. Germain zinasema kuwa mshambulizi Neymar atahitaji kufanyiwa upasuaji kuharakisha uwezekano wake wa kupona ili kushiriki kombe la dunia linaloanza mwezi Juni. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Neymar

Hata hivyo kocha wa PSG Unai Emery alikana kuwa Neymar atafanyiwa upasuaji akiongeza kuwa anaweza bado kucheza mechi ya Champions League dhidi ya Real Madrid tarehe 6 Machi. (Mundodeportivo - in Spanish)

Juventus wana mpango wa kufanya mazungumzo na maajenti wa kiungo cha kati wa Liverpool Emre Can, 24, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Stefan de Vrij

Liverpool wamekuwa katika nafasi nzuri ya kumsaini mchezaji wa Napoli mzaliwa wa Brazil Jorginho. (Star)

Arsenal sasa wameanza kumsaka mlinzi wa Atletico Madrid raia wa Urugauy Jose Maria Gimenez, 23, baada ya kukiri kuwa wameshindwa katika kumwinda mholanzi Stefan de Vrij. (Sports Illustrated)