Kamati ya Olimpiki yaiondolea adhabu Urusi

Adhabu hiyo ilianza mwezi Disemba mwaka jana
Image caption Adhabu hiyo ilianza mwezi Disemba mwaka jana

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki imeondoa kwenye kifungo Urusi.

Katika taarifa yake imesema adhabu ya Urusi imeondolewa mara moja kuanzia sasa.

Adhabu hiyo ilianzia Disemba mwaka jana baada ya wanariadha wa Urusi kugundulika kutumia dawa zilizokataliwa michezoni mwaka 2014, michuano iliyofanyika katika mji wa Sochi.

Inadaiwa kuwa serikali ya Urusi ilifadhili mpango huo kwa kiasi kikubwa.

Image caption Rais wa Urusi Vladimir Putin akifurahia jambo na wanamichezo wa nchi yake

Wanariadha wa Urusi katika michuano ya mwaka huu iliyofanyika Pyeongchang, iliwabidi washiriki bila kupeperusha bendera ya nchi yao.

Wawili kati yao walishindwa kushiriki baada ya kugundulika kutumia dawa hizo.

Siku ya Jumapili OIC ilipiga kura kuondoa adhabu kwa Urusi iwapo wanariadha wake wataacha kabisa kutumia dawa hizo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii