Nahodha wa klabu ya Fiorentina Davide Astori afariki dunia

Davide Astori Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Astori ameichezea Fiorentina mechi 27 msimu huu

Nahodha wa Fiorentina raia wa Italia Davide Astori amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 31.

Mlinzi huyo alifariki kutokana na ugonjwa wa ghafla, kwa mujibu wa klabu yake kupitia akaunti yao wa Twitter.

Fiorentina walipangiwa kucheza na Udinese leo jioni kwenye ligi ya Serie A lakini mechi hiyo imefutwa.

Astori ambaye aliichezea Italia mara 14, alijiunga na Fiorentina mwaka 2016 akitokea Cagliari na kuwachezea mara 58.

Cagliari walihairisha mechi dhidi ya Genoa leo asubuhi.

Astori ambaye ana mke na mtoto msichana wa miaka miwili, aliichezea AC Milan ujanani kabla ya kujiunga na Cagliari mwaka 2008.

Aliicheza klabu hiyo kwa miaka minane na akacheza kwa mkopo kwenye vilabu vya Roma na Fiorentina kabla ya kuelekea Fiorentina kwa mkataba wa kudumu miaka miwili iliyopita.

Meneja wa zamani wa Fiorentina Roberto Mancini alisema: "Nimehusunishwa sana kutokana na kile kimemfanyikia Davide Astori, rambi rambi zangu ziendee familia yake."

AC Milan walisema katika taarifa: "Mwanamume ambaye alipenda kandanda na ambaye alikuwa kama mcheza kandanda nasi. AC Milan imeshutushwa na kifo cha Davide Astori.

Mada zinazohusiana