Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 06.03.2018

Hazard Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Chelsea Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 27, anasua sua katika kusaini kandarasi mpya na klabu hiyo kwa matumaini kwamba mabingwa wa Uhispania Real Madrid watamuwania. (Mail)

Beki wa Arsenal Hector Bellerin amemkasirikia meneja Arsene Wenger baada ya kutemwa katika mchuano dhidi ya Brighton Jumapili wakati kikosi kamili katika mechi hiyo kilitangazwa saa mbili kabla ya kipenga kupulizwa. (Sun)

Manchester City, Manchester United na Arsenal wametuma wajumbe wakamtizame mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Italia anayeichezea Napoli kwa thamani ya £ milioni 60 Jorginho. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mauricio Pellegrino

Southampton itamfuta kazi meneja Mauricio Pellegrino mwishoni mwa msimu hata wakiponea katika ligi ya England.

Kiongozi wa Fulham Slavisa Jokanovic na wa FK Ostersunds Graham Potter ndio wanaopigiwa upatu kuichukuwa nafasi yake. (Mirror)

Mkurugenzi mtendaji wa West Brom Mark Jenkins ameelekea China kukutana na mmiliki wa Baggies Guochuan Lai na anatarajiwa kuhojiwa kumhusu meneja Alan Pardew. (telegraph)

Mchezaji wa Brazil wa kiungo cha kati Ramires, mweny umri wa miaka 30, angependa kujiunga na Chelsea, miaka miwili baada ya kuondoka katika timu hiyo kujiung na klabu ya Uchina Jiangsu Suning. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Haijkuwa rahisi kwa Kante kufika alipofika leo lakini amejizatiti pakubwa

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka 26, amezimia na kupoteza fahamu katika uwanja wa mazoezi wa Cobham siku ya Ijumaa lakini utafiti wa kimatibabu kutoka kwa daktari wa moyo wa timu ya taifa ya Ufaransa umedhihirisha kwamba yuko salama. (Telegraph)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Nice Mario Balotelli anatamani kuingia Juventus au Napoli huku mchezaji huyo mwenye umri wamiaka 27 akitarajiwa kuitwa upya katika kikosi cha Italia. (La Domenica Sport, via Mail)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Racing Club Lautaro Martinez anatarajiwa kujiunga na Inter Milan, licha ya mchezaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 kulengwa na Arsenal na Barcelona. (Sport Mediaset, via Talksport)

Stoke City na Lazio wanamuawania mchezaji wa kiungo cha kati wa Uhispania anayeichezea Real Betis Fabian Ruiz. (Mundo Deportivo, via Talksport)

Watford ni miongoni mwa vilabu vya ligi ya England vinavyomwinda mlinzi wa Stevenage mwenye umri wa miaka 18 Ben Wilmot. (Watford Observer)

Mada zinazohusiana