Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

SIMBA SC

Tatizo la Miundo mbinu katika viwanja vya michezo limeendelea kuwa ni kero kwa wadau wa michezo hususani mchezo wa soka , baada ya jana usiku kulazimika kusitishwa kwa muda mechi ya kombe la shirikisho kati ya Timu ya Simba sc na El Masri ya Misri iliyochezwa katika uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam.

Umeme ulikatika wakati mchezo ukiwa unaendelea kutokana na kunyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali .

Kwa mujibu wa sheria za soka waamuzi wa mchezo huo Hando Helpus akisaidiwa na Zakjele Thusi na Athenkosi Ndongeni wote kutoka Afrika, walilazimika kusitisha mchezo zikiwa zimesalia dakika 7 mchezo kumalizika ikiwa ni dk 83 kipindi cha pili kutokana na uwanja kujaa maji na kugubikwa na giza totoro.

Hadi mchezo ulipositishwa matokeo ilikuwa mabao 2-2 na baadaye wasimamizi wakachezesha dakika zilizosalia kumaliza mechi hiyo wakai hali ilipotulia kiasi.

Licha ya Baadhi ya viwanja vikubwa vya michezo kuidhinishwa kutumika kwa mashindano mbalimbali ya mpira wa miguu, viwanja hivyo vimekosa kukidhi vigezo vya usalama vya shirikisho la soka Ulimwenguni (Fifa).

katika uchunguzi uliofanyika na kubaini hata hivyo wamiliki wa viwanja mbalimbali Afrika wamekuwa wakitumia fedha za mgawo wa mapato ya mechi kwa shughuli za kiutawala badala ya kuboresha viwanja ili kukidhi matakwa ya kanuni za usalama za Fifa.

Mada zinazohusiana