Arsenal wawalima Watford 3-0

Mustafi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ushindi huo unaiweka Arsenal nafasi ya sita, pointi 10 nyuma ya nafasi ya nne Tottenham.

Arsenal imemaliza kipindi cha kushindwa mfululizo katika Premier League kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Watford.

Shkodran Mustafi alitumbukiza wavuni free-kick ya Mesut Ozil kuwapa Gunners bao la kwanza dakika ya nane kabla ya Pierre-Emerick Aubameyang kutumbukiza pasi yake Henrikh Mkhitaryan bao la pili.

Watford walikuwa na fursa nzuri wa kufunga kupitia penalti lakini mkwaju wake Troy Deeney ukazuia na Petr Cech.

Mkhitaryan aligonga msumari wa mwisho kwa jeneza lake Watford na kuipa Arsenal ushindi wa kwanza tangu wawalime Everton 5-1 tarehe tatu Februari.

Ushindi huo unaiweka Arsenal nafasi ya sita, pointi 10 nyuma ya nafasi ya nne Tottenham.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watford walikuwa na fursa nzuri wa kufunga kupitia penalti lakini mkwaju wake Troy Deeney ukazuia na Petr Cech.

Mada zinazohusiana