Edmund atupwa nje Paribas Open na Dudi Sela

Edmund amesema anajipanga kwa ajili ya michuano ya Miami Open
Image caption Edmund amesema anajipanga kwa ajili ya michuano ya Miami Open

Mchezaji namba moja kwa tennis nchini Uingereza Kyle Edmund, ametupwa nje ya michuano ya Paribas Open baada ya kuchapwa 6-4 6-4 na Dudi Sela wa Israel.

Edmund, 23, alianza kwa makali lakini hatimaye akashindwa kufurukuta.

Sela, 32, anashika nafasi ya 97 duniani na amesema alitumia uzoefu wake wote kumkabili Edmund.

Kwa sasa Edmund anatarajiwa kupeleka nguvu zote kwenye michuano ya Miami Open baadae mwezi huu.

Edmund alichukua nafasi ya Andy Murray kama mchezaji wa kwanza kwa tennis nchini Uingereza kwa upande wa wanaume.

Sela atakutana na Marcos Baghdatis wa Cyprus ama Diego Schwartzman kutoka Argentina katika hatua ya 6 bora.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii