Tetesi za soka Ulaya Jumatano 14.03.2018

Mchezaji wa Brazil na Shaktar Donetsk Fred
Image caption Mchezaji wa Brazil na Shaktar Donetsk Fred

Huenda Manchester City wakashindwa kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Shakhtar Donetsk mwenye umri wa miaka 25 Fred, ambaye anasakwa na Manchester United.(Times - subscription required)

Southampton wanatumai watamsajili mkufunzi Mark Hughes kuwa meneja wao mpya siku ya Jumatano. Mkufunzi huyo wa zamani wa Stoke amepewa kandarasi hadi mwisho wa msimu huu. . (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere

Everton wana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Jack Wilshere kwa uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Liverpool ina hamu ya kutaka kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig mwenye umri wa miaka 22 Timo Werner. (Independent)

Image caption Liverpool ina hamu ya kutaka kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig mwenye umri wa miaka 22 Timo Werner. (Independent)

West Ham itamuajiri mkurugenzi wa soka mwisho wa msimu huu kwa lengo la kuimarisha mipango yake ya uhamisho , swala ambalo halijawafurahisha mashabiki wake. (Evening Standard)

Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis anamtaka mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama kocha mpya wa klabu hiyo. (Daily Star)

Image caption Ivan Gazidis kushoto na Arsene Wenger kulia

Mshambuliaji wa Middlesbrough mwenye umri wa miaka 26 na raia wa Denmark Martin Braithwaite anataka kuandikisha mkataba wa kudumu na klabu ya Bordeaux baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo msimu huu. (Evening Gazette, via Gold FM)

Image caption Harry Kane apata jeraha

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane hatoshiriki katika mechi hadi mwezi Mei baada ya ukaguzi kuonyesha kuwa alipata jeraha la kifundo cha mguu zaidi ya alivyodhaniwa hapo awali. (Mirror)

Crystal Palace iko tayari kuuza haki zake za jina la uwanja wake wa Selhurst Park ili kuisaidia kujenga uwanja mpya utakaogharimu pauni milioni moja. (Evening Standard)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii