Timu ya Besiktas imeshtakiwa na UEFA baada ya paka kuingia uwanjani

Ginger cat on the pitch in Turkey Haki miliki ya picha EPA
Image caption Paka aliyetunukiwa kuwa mchezaji bora

Timu ya Besiktas imeshtikiwa na UEFA baada ya paka kuingia uwanjani wakati mchezo kati yao na Bayern Munich.

Mwamuzi wa mpira Muingereza Michael Oliver alisimamisha mechi wakati kipindi cha pili cha mchezo kwenye uwanja wa Vodafone Park hadi paka huyo alipotoka.

Mashtaka hayo yameelezwa kuwa ni "ukosefu wa mpangilio" wakati pia klabu hiyo ya Uturuki ilishitakiwa kwa "kutupa vitu uwanjani na kuziba ngazi"

Kesi hiyo itasikilizwa na bodi ya UEFA tarehe 31 Mei.

Mashabiki wa klabu hiyo ya Ujerumani walimchagua paka huyo kuwa 'mchezaji bora wa mechi'

Haki miliki ya picha Bayern Munich

Lakini kumekuwa na visa vingine vya kustaajabisha kwenye uwanja wa soka:

"Kuingia uwanjani na bastola"

Timu ya Ugiriki walifukuzwa kwa muda baada ya rais wa timu ya PAOK kuingia uwanjani akiwa na bastola wakati wa mechi Jumapili iliyopita.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Savvidis aliingia uwanjani akiwa na bastola kiunoni

Ivan Savvidis, aliyekuwa ametundika bastola hiyo kiunoni alikuwa akijaribu kuongea na mwamuzi wa mpira baada ya goli la timu yake dhidi ya AEK Athens kufutwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Savvidis aliingia uwanjani akiwa na bastola kiunoni

'Kukimbia wakiwa uchi'

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bath play their home matches at the Recreation Ground

Wachezaji wa timu ya Bath waliadhibiwa baada ya kukimbia wakiwa uchi kwenye uwanja wakati wa mazoezi, Mei mwaka jana.

Mada zinazohusiana