Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 17.03.2018

Lewandowsk huenda akajiunga na Real madrid katika dirisha kubwa la usajili
Image caption Lewandowsk huenda akajiunga na Real madrid katika dirisha kubwa la usajili

Real Madrid imekubali kusajili mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland Robert Lewandowski.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 pia anafuatiliwa na klabu za Chelsea na Manchester United.(Mundo Deportivo )

Mlinzi wa kati wa Real Madrid Raphael Varane amesema Manchester United inamuhitaji. Mfaransa huyo mwenye miaka 24 alisajiliwa klabuni hapo chini ya Jose Mourinho.(Cadena Ser, via Sun)

Kiungo wa zamani wa Liverpool na Bayern Munich Dietmar Hamann amesema Bayer wanazungumza na kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino juu ya uwezekano wa kuwanoa.(Sky, via Mirror)

Image caption Jack Wilshare yuko katika mawindo ya Everton

Everton iko tayari kumlipa kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ambaye mkataba wake na Gunners unaisha mwisho wa msimu huu.Wapo tiyari kumpa paundi milioni 8 kwa mwaka iwapo atasajiliwa bure.(Times )

Borussia Dortmund wameonyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Westham mreno Domingos Quina.(Sun)

Spurs wanatarajia kufanya mazungumzo ya kumpa mkataba mpya mshambuliaji raia wa Korea Kusini Son Heung-min.Mkataba wake wa sasa unaishia mwaka 2020.(Sky Sports)

Image caption Michael Appleton kuwanaowaniwa na West Brom

Meneja msaidizi wa Leicester city Michael Appleton yupo miongoni mwa makocha wanaowaniwa na West Brom kuziba nafasi ya Alan Pardew.(Telegraph)

Mlinda mlango wa Roma Alisson anahusishwa kujiunga na Liverpool lakini matamanio yake ni kwenda Real Madrid.(Express)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema mlinzi wa kati Gary Cahill na mshambuliaji Alvaro Morata wanahitaji juhudi zaidi iwapo wanataka kurejea katika kikosi cha kwanza na kuweka uwezekano wa kuziwakilisha timu zao za taifa ambazo ni Uingereza na Hispania.(Express)

Conte anaamini hawezi ondolewa kwenye klabu ya Chelsea iwapo mabingwa hao wa msimu uliopita hawatafuzu kucheza klabu bingwa ulaya msimu ujao.(Telegraph)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii