Tetesi za soka Ulaya Jumapili 18.03.2018

kocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption kocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique
Arsene Wenger wa Arsenal Haki miliki ya picha Empics
Image caption Arsene Wenger wa Arsenal

Mkufunzi wa zamani wa Barcelona Luis Enrique amezuia kuandikisha mkataba na Chelsea huku akisubiri kitakachotokea katika klabu ya Arsenal. (Sunday Star)

Image caption Neymar amezua wasiwasi katika klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain baada ya kusema 'miezi mitano' katika klabu hiyo ni sawa na miaka mitano katika klabu hiyo tangu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ajiunge na klabu hiyo kutoka Barcelona kwa dau la rekodi ya £200m msimu uliopita. (UOL Esporte, via Sunday Express)

Neymar amezua wasiwasi katika klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain baada ya kusema 'miezi mitano' katika klabu hiyo ni sawa na miaka mitano katika klabu hiyo tangu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ajiunge na klabu hiyo kutoka Barcelona kwa dau la rekodi ya £200m msimu uliopita. (UOL Esporte, via Sunday Express)

Neymar ambaye anauguza jeraha anataka mshahara wake kuongezwa ili kusalia PSG msimu ujao.. (Sunday Times - subscription required)

Image caption Mkufunzi wa PSG Unai Emery amefunguka kuhusu uvumi wa Neymar kujiunga na Real Madrid

Mkufunzi wa PSG Unai Emery amefunguka kuhusu uvumi wa Neymar kujiunga na Real Madrid akisema kuwa kuna uwezekano akajiunga na klabu hiyo (Sun on Sunday)

Liverpool inataka kumsajili kipa wa Roma Alisson anayedaiwa kuwa na thamani ya £70m , lakini Real Madrid wanapigiwa upatu kumsajili mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25. (Sunday Mirror)

Image caption Julian Draxler

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp pia anajaribu kuishawishi bodi ya klabu hiyo kumsajili winga wa Ujerumani na PSG Julian Draxler, 24, mwisho wa msimu huu. (Sunday Express)

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Hatma ya Paul Pogba haijulikani Manchester United

Hatma ya Paul Pogba katika klabu ya Manchester United haijulikani huku ajenti wa mchezaji huyo Mino Raiola, akidaiwa kuisaka klabu itakayomnunua mchezaji huyo ,25 (Sunday Mirror)

Image caption Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa Mohamed Salah anakaribia kulinganishwa na Lionel Messi baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Watford.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa Mohamed Salah anakaribia kulinganishwa na Lionel Messi baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Watford.

Image caption Fred

Manchester City inatarajiwa kuipiku Manchester United katika kumsajili kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk na raia wa Brazil Fred. (Sunday Star)

Image caption Romelu Lukaku anasema kuwa Man United kuwasajili wachezaji bora mwisho wa msimu

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, 24, anasema kuwa anajua kwamba wachezaji wengi watasajiliwa na klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Mail on Sunday)

Image caption Son Heung-min,

Tottenham inatarajiwa kumpatia mshambuliaji wake Son Heung-min, 25, mkataba mpya ulioimarika kama zawadi ya mchezo wake mzuri msimu huu(Talksport)

Image caption Zinedine Zidane amepinga madai kwamba huenda mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 28, hana raha kuichezea Real Madrid. (Mail on Sunday)

Zinedine Zidane amepinga madai kwamba huenda mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 28, hana raha kuichezea Real Madrid. (Mail on Sunday)

Image caption Eden Hazard

Antonio Conte amepnga madai kwamba Chelsea huenda ikawakosa wachezaji kama vile Eden Hazard, 27, iwapo klabu hiyo itashindwa kushiriki katika kombe la vilabu bingwa msimu ujao.. (London Evening Standard)

Beki wa zamani wa Chelsea John Terry, 37, anataka kuichezea klabu ya daraja la kwanza msimu ujao Aston Villa hatua inayomaanisha kwamba huenda akarudi kushiriki katika ligi kuu ya Uingereza. (People)

Mada zinazohusiana