Je Mo Salah anakaribia kumrithi Messi?

Mohamed Salah kushoto na mshambuiaji wa Barcelona nyota Lionel Messi kulia Haki miliki ya picha Reuters/Getty images
Image caption Mohamed Salah kushoto na mshambuiaji wa Barcelona nyota Lionel Messi kulia

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa Mohamed Salah anakaribia kulinganishwa na Lionel Messi baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Watford.

Salah ndiye anayeongoza kwa mabao katika ligi tano bora za Ulaya akiwapiku Lionel Messi wa Barcelona na Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane.

Lakini kulingana na Klopp mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Misri ananedelea vyema.

''Sidhani kwamba Mo anataka kufananishwa na Lionel Messi'', alisema.

''Messi amekuwa akifanya kile anachofanya kwa zaidi ya miaka 20 iliopita'' .

Machezaji wa mwisho aliyekuwa na ushawishi kama huo kwa timu yake alikuwa Diego Maradona.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mohamed Salah akifunga bao lake dhidi ya Watford siku ya Jumamosi

Lakini Mo ni ''mchezaji mzuri sana , kwa kweli''.

''Katika maisha yako iwapo unataka kuonyesha kile unachoweza kufanya lazima iwe mara kwa mara , na hilo amefanikiwa kuonyesha''.

Akiwa amewasili Liverpool chini ya miezi tisa pekee , Salah ameifungia timu hiyo magoli 36 ikiwa ni mabao mengi kutoka kwa mchezaji mmoja katika msimu wa kwanza katika uwanja wa Anfield, ikiwa imesalia mechi saba katika ligi ya Uingereza msimu huu.

Nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard anaaamini kwamba : Tunashuhudia mwanzo wa mchezaji bora.

Na mchezo wake umeanza kuimarika katika hali ya kwamba magoli yake yameanza kufanana na yale ya Messi.

Ilimchukua dakika nne pekee kufunga bao la kwanza dhidi ya Watford , akiwachenga mabeki wa Hornbets na kumuacha beki Miguel Btitos chini kabla ya kufunga.

Goli hilo lilifanana kama lile la Messi dhidi ya Bayern Munich katika kombe la vilabu bingwa la 2015 wakati alipomuacha Jerome Boateng akiwa ameanguka.

Lakini Salah anasalia mkimya kuhusu kipawa chake, akiwashukuru wachezaji wenzake na kusema kuwa 4-0 dhidi ya kikosi cha Javi Gracia ni muhimu sana.

''Mo ni mchezaji mzuri sana huo ni ukweli.Wachezaji wangu hupendelea kushirikiana naye na anapenda kushirikiana nao''.

Image caption Wachezaji wenye magoli mengi katika ligi tano za Ulaya

Akiwa na umri wa miaka 25 Salah ana kibarua kigumu kuafikia yale yalioafikiwa na Messi.

Alishiriki katika mechi tatu za ligi ya Uingereza akiichezea Chelsea wakati ambapo klabu hiyo ilishinda ubingwa wa ligi 2015, pia alikuwa miongoni mwa kikosi cha Basel cha 2012 na 2014 wakati klabu hiyo iliposhinda mataji ya ligi.

Winga huyo pia aliisaidia Misri kushiriki katika kombe la dunia baada ya robo karne wakati alipofunga bao la dakika 95 kwa njia ya penalti katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Congo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lakini Messi ambaye baadhi wanasema alishiriki katika timu bora ya Barcelona alishinda mataji sita

Lakini Messi ambaye baadhi wanasema alishiriki katika timu bora ya Barcelona alishinda mataji sita , matatu ya vilabu bingwa na medali ya dhahabu ya Olimpiki alipokuwa na umri wa miaka 25.

Pia ameshinda taji la mchezaji bora duniani mara 5.