Cristiano Ronaldo afunga hat-trick yake ya 50

Cristiano Ronaldo afunga hat-trick yake ya 50 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cristiano Ronaldo afunga hat-trick yake ya 50

Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick yake ya 50 tangu aanze kucheza soka ya kulipwa huku Real Madrid ikiilaza Girona na hivyobasi kupanda hadi nafasi ya tatu katika ligi ya La Liga.

Ronaldo alifunga krosi ya Toni Kroos lakini kichwa cha Cristhian Stuan kilifsawazisha na kufanya mambo kuwa 1-1

Real hatahivyo ilichukua uongozi kufuatia shambulizi kali la Ronaldo kabla ya kumpatia krosi Lucas Vazquez aliyefunga bao la tatu na hatimaye nyota huyo akakamilisha hat-trick yake.

Stuani alifunga bao la pili la Girona, Gareth Bale alifunga la tano , kabla ya Juanpe kuifungia Girona bao la tatu lakini Ronaldo alipata bao lake la nne na la sita katika muda wa majeruhi.

Matokeo hayo yanaiweka Real Madrid juu ya Valencia lakini wako pointi nne nyuma ya Atletico Madrid ambao walilazwa 2-1 na Vilareal.

Real wako pointi 15 nyuma ya viongozi wa ligi Barcelona ambao walishinda 2-0 dhidi ya Athletico Bilbao siku ya Jumapili.

Mada zinazohusiana