Jose Mourinho: Mkufunzi wa Manchester United anaonekana kupitwa na wakati - Chris Sutton

Jose Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mourinho amekosolewa vile anavyofanya kazi katika klabu ya Man United

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaonekana kupitwa na wakati na tabia zake zimebadilika , kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton.

Mourinho amekosolewa na baadhji ya mashabiki wa United pamoja na wachanganuzi wa kandanda kwa mtindo wake wa kucheza kandanda unaoonekana kutokuwa na mbinu mpya.

United iko katika nafasi ya pili katika ligi ya Uingereza na wako katika nusu fainali katika kombe la FA lakini walibanduliwa katika kombe la vilabu bingwa wiki iliopita.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright aliambia BBC Radio 5 live asingependelea kucheza chini ya Mourinho hivi sasa.

United wako pointi 16 nyuma ya Manchester City katika ligi huku kukiwa imesalia mechi nane na itachuana na Tottenham mwezi ujao ili kufika fainali ya kombe la FA.

Lakini huku City ikiwa imefanikiwa kufunga mabao 85 katika ligi ya Uingereza msimu huu , United imefunga mabao 58 pekee, ikiwa ndio machache zaidi miongoni mwa timu nne bora katika ligi hiyo kulingana na jedwali.

Red Devils walibanduliwa katika kombe la Ulaya na Sevilla, walioshinda 2-1 katika uwanja wa Old Trafford huku City na Liverpool zikisonga mbele katika robo fainali.

Sutton akizumnguza siku ya Jumatatu alisema: Mourinho amebadilika yeye binafsi kutoka alivyokuwa 2004. Anaangazia maswala madogo ya kijinga. Je ni janga kwa Man United kwa sasa? Hapana.

Lakini hilo ndio lililokuwa lengo la Mourinho kuja Man United na kumaliza nyuma ya City na kutokuwa na ari ya kuwania mataji makubwa? amepitwa na wakati.

Anaangalia City na mtindo wa soka wao na Liverpool .Huyu ni mtu ambaye alisajiliwa na Man United kwa kuwa alikuwa anaonekana kuwa na kipaji , Sasa anaonekana amepitwa na wakati kutokana na mtindo wa mchezo wake na vile timu nyengine zinavyocheza.

Image caption Didier Drogba ni miongoni mwa wachezaji ambao wanadaiwa kutokuwa na raha katika Old Trafford

Mourinho mwenye umri wa miaka 55 alishinda ligi ya Uingereza mara tatu , mara mbili akiwa mkufunzi wa Chelsea.

Alimrithi Louis van Gaal kama mkufunzi wa United mnamo mwezi Mei 2016 na ameshinda kombe la EFL pamoja na lile la Yuropa katika msimu wake wa kwanza .

Wright anamlaumu mkufunzi huyo kwa kuleta kiza katika klabu hiyo .

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza alisema: Sijui amefanywa nini. Klabu hiyo ilimleta Mourino ili kuleta ubora ,ametumia fedha nyingi lakini anazozana na kila mtu.

Manchester City inacheza mtindo wa kandanda ambao ni mzuri na unaonekana .

Je Shaw ananyanyaswa?

Baada ya United kufunga huku mashambulio yao yote yakilenga goli wakati walipoishinda Brighton 2-0 katika raundi ya sita kombe la FA siku ya Jumamosi, Mourinho alisema kwamba kikosi chake kiliogopa kucheza.

Beki wa kushoto Luke Shaw alikuwa mmoja ya wachezaji waliotajwa na kukosolewa na mkufunzi huyo baada ya kusema kwamba hakufurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa UIngereza ambaye ameichezea United mara 15 msimu huu alikuwa akianzishwa tangu Februari.

Je Ananyanyaswa? aliuliza Sutton. Sipendelei neno 'kunyanyaswa' katika soka kwa sababu huwa kuna hisia kali katika chumba cha maandilizi hususan kutoka kwa mkufunzi.

Huwa kuna maneneo yanayotumiwa na mkufunzi kuwakosoa wachezaji.

Swala hilo limekuwa likifanyika tangu soka ianze. Kila mtu yuko tofauti. Kwa upande wa ukufunzi wana haki ya kuhakikisha kuwa wanafahamiana na kila mchezaji kitabia.

Wright alisema kuwa Mourinho anafaa kufanya kila kitu ili kuhakikisha kuwa kiwango cha mchezo wa Luke Shaw kinaimarika baada ya mchezaji huyo kuvunjika mguu wake wa kulia mara mbili mwezi Septemba 2015.

Alisema: Alivunjika mguu na sasa anaonekana mzito lakini hilo halimaanishi kwamba hawezi kupanda juu na kushuka chini katika wingi yake.

Sijui maisha yake ya kibinafsi lakini haiwezekani kwamba kila mara mkufunzi anarudi kumkumbusha. Mourinho anafaa kumuimarisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye huenda atashiriki katika kombe la dunia na kikosi cha Uingereza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mourinho alisema mwezi Aprili kwamba Shaw alitumia mwili badala ya akili yake wakati wa memchi ya 1-1 dhidi ya Everton

Kulingana na mwandishi wa BBC Sport's Simon Stone katika BBC Radio 5 live:

Ukosoaji wa Mourinho umemuudhi Shaw. Amekasirishwa na hatu hiyo . Siwezi kusema sana kuhusu vile watu wake walivyokasirishwa.

Ni hivi juzi alikuwa akiuguza jeraha la mguu na sio mara ya kwanza kwamba Mourinho amemkosoa , wengine huweka vichwa vyao chini lakini inadaiwa kuwa ilikuwa kibinafsi.

Michael Carrick amekuwa United kwa takriban miaka 12-13 na anatarajiwa kujiunga na idara ya ukufunzi ya timu hiyo. Iwpao kuna mtu anayefaa kumteta Shaw basi inafaa kuwa Carrick.

Ni vyema kuona mabao yatakavyokuwa. Sio chumba cha maandilizi cha miaka minne ama mitano iliopita wakati kulikuwa na wachezaji kama vile Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand ambao wangeweka kikao na Furgusson na kumwambia kuna swala tata.

Mada zinazohusiana